Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akivishwa skafu na vijana wa
skauti mara baada ya kuwasili katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.
|
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mhe. John Palingo mara baada ya kuwasili katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, Mkoani Kilimanjaro |
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Viongozi na wakazi
wa Marangu wakati wa hafla ya kuwaaga vijana watakaopanda
Mlima Kilimanjaro ikiwa ni kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 ya Kifo cha Baba
wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
|
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi akufafanua jambo kuhusu ushiriki wa vijana hao watakaopanda Mlima Kilimanjaro, Machi 26, 2019. |
Baadhi ya watumishi wa Hifadhi
ya Mlima Kilimanjaro wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara ya kuwaaga vijana hao.
Vijana wanaotarajiwa kupanda
Mlima Kilimanjaro wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika
Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama kabla
ya kuanza safari ya kupanda mlima huo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,
Mhe. Jenista Mhagama akikabidhi Bendera ya Taifa kwa vijana watakaopanda Mlima
Kilimanjaro ikiwa ni kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 ya Kifo cha Baba wa
Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,
Mhe. Jenista Mhagama akifurahia jambo wakati wa kuwaaga vijana kabla ya kuanza
zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,
Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali,
Uongozi wa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na Vijana watakaopanda Mlima
Kilimanjaro.
PICHA
ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI,
VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
|
Na; OWM – KVAU, Kilimanjaro
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama amewahimiza vijana kuwa wazalendo na kuithamini nchi yao.
Akizungumza wakati wa hafla ya
kuwaaga vijana waliopanda Mlima Kilimanjaro jana tarehe 26 Machi, 2019 Mkoani Kilimanjaro ikiwa ni
kuaadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius
Kambarage Nyerere.
Waziri Mhagama alisema kuwa,
Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere alikuwa kiongozi
mzalendo kwa nchi yake na alijali utu na usawa, hivyo ni vyema vijana na vizazi
vijavyo wakarithishwa falsafa za Baba wa Taifa.
“Vijana mna kila sababu kuyaenzi
matendo ya Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere na Mhasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar,
Abeid Amani Karume kwa vitendo kwa kuwa ninyi ndio nguzo ya Taifa na mnaelewa
vema tulipotoka, tulipo na tunapoenda,” alisema Mhagama
Aliongeza kuwa, Viongozi hawa
hawakuwa wabinafsi kwa kujilimbikizia mali na hawakubagua mtu kwa rangi wala
kabila bali walijenga Taifa na kudumisha amani na moja.
Aliendele kwa kuwapongeza
vijana kwa azma yao ya kuenzi historia na mazuri yaliyofanywa na viongozi hao
kwa kupanda mlima Kilimanjaro na kuwatakia baraka waende na kurudi salama.
“Kitendo hiki ni cha kishujaa
na uzalendo wa hali ya juu kwa Taifa ikiwa ishara ya kumuenzi Baba wa Taifa,”
alieleza Mhagama
Aidha Waziri Mhagama alitoa
rai kwa vijana kuwa wazalendo na kuwasihi wafanye kazi kwa bidii ili kujenga Taifa
kupitia uchumi wa viwanda utakao ifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati
ifikapo mwaka 2025.
Alifafanua kuwa uzalendo
lazima ujengwe sambamba na ujenzi wa uchumi wa Taifa, ulinzi na usalama wa Taifa
na utunzaji wa tunu za Taifa.
Pamoja na hayo, aliwapongeza
na kuwashukuru Viongozi wa Mkoa wa Songwe na Lindi pamoja na uongozi wa Hifadhi
ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) kwa ushirikiano mkubwa na Ofisi yake katika kuwashirikisha
vijana kwenye suala hilo.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya
ya Moshi, Mhe. Kippi Warioba alisema kuwa tukio hili ni muhimu kwa vijana
kutambua historia na mchango wa Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere katika Taifa.
“Tumieni fursa hii kupitia
vitabu mbalimbali vya kihistoria ili mjifunze mipango, mwenendo na malengo ya Baba
wa Taifa itawasaidia na kuwajengea nafasi nzuri ya kujitambua na kuelewa
historia ya Taifa,” alisema Warioba.
Naye Mkurugenzi wa Maendeleo
ya Vijana, Bw. James Kajugusi alieleza kuwa Baba wa Taifa alianza harakati za
kulikomboa Taifa akiwa kijana na aliendelea kufanya hivyo kwa kuwa hamasisha
vijana kujenga Taifa lao baada ya kupata uhuru.
MWISHO
Post A Comment: