Watalii wa ndani wakifurahia Mazingira mazuri ya HIfadhi ya Msitu wa Mazingira Asilia Amani 
Watalii wakiwa wanafurahia safari yao ya kutalii katika hifadhi ya mazingira asilia ya amani

Mtendaji MKuu wa Wakala wa Huduma za MIsitu Tanzania Prof Dos Santos Silayo (wa kwanza kulia anayeshika maji) akifurahia maji yanayotiririka kwenye maporomoko ya maji yaliopo ndani ya Hifadhi za Mazingira Asilia-1
Muheza – Tanga

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania - TFS imeendelea kuhakikisha kwamba Sekta ya Utalii katika Hifadhi za Misitu Asilia nchini inaimarishwa na kuendelezwa kwa kuwa ni moja ya sekta zinazochangia kwa kiasi kikubwa katika Pato la Taifa na ajira kwa wananchi pamoja na uhifadhi wa misitu hiyo. 

Mtendaji Mkuu wa TFS, Profesa Dos Santos Silayo amesema hayo jana alipotembelea Hifadhi ya Msitu wa Mazingira Asili Amani wilayani hapa na kujionea changamoto mbalimbali ikiwamo idadi ndogo ya vitanda kwa ajili ya malazi.“TFS inasimamia utekelezaji wa mikakati ya kukuza utalii nchini kwa kuongeza msukumo katika utalii wa ikologiakwa kuboresha miundombinu kwenye maeneo ya Hifadhi ya Msitu wa Mazingira Asilina kuyatangaza maeneo hayo.

“Kuhamasisha wananchi kutembelea vivutio vya utalii wa ndani, mfano mwaka huu tulitoa ofa katika maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba)kutembelea Msitu huu wa Hifadhi ya Mazingira Asilia ya Amani na watu wengi walijitokeza kujionea vivutio vingi wakiwamo vinyonga wenye pembe tatu.Profesa Silayo anaongeza kuwa kutokana na Msitu wa HIfadhi ya Mazingira Asilia Amani kuwa na vivutio vingi, wameweka mazingira yatakayowezesha wawekezaji wa ndani kuendeleza biashara za utalii pamoja na kuwajengea uwezo waongoza watalii.

Mtendaji huyo anasema tayari wameshatangaza tenda kwa wawekezaji wenye nia ya kuwekeza kwenye malazi na shughuli mbalimbali za utalii kwenye hifadhi ya Amani na sasa wako kwenye hatua za mwisho za kumpata mzabuni.Mhifadhi wa Hifadhi ya Hifadhi ya Mazingira ya Amani, Mwanaidi Kijazi anasema pamoja na mambo mengine, mkakati huo umefunguafursa za utalii mkoani Tanga na kujenga mazingira bora kwa wawekezaji binafsi kuweza kujenga hoteli za kisasa za kulala wageni ikiwamo usafiri wa kufikisha wageni katika maeneo hayo.

Mhifadhi huyo anasema wanashirikiana kuhifadhi msitu huo kwa kuishirikisha jamii kutumia mazingira asilia ya msitu huo kama chanzo cha kujipatia kipato kwa kutoa elimu ya ujasiriamali, kutenga maeneo ya biashara, kuishirikisha sekta binafsi na kutoa elimu ya uhifadhi kwa umma. 

Aidha, Kijazi amesema katika mwaka wa fedha wa 2017/2018 wamefanikiwa kuingiza shilingi milioni 59.2 kutokana na wageni 782 waliotembelea hifadhi hiyo.Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 2015 inaielekeza Serikali kuongeza idadi ya watalii wanaoingia nchini kutoka 1,102,026 mwaka 2015 hadi 2,000,000 mwaka 2020 kwa kuwezesha Sekta Binafsi kuwekeza katika huduma za miundombinu ya utalii pamoja na kuendeleza Mkakati wa Kimataifa wa Utangazaji wa Utalii ili kuwavutia watalii wengi zaidi.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: