Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,  Profesa Makame Mbarawa amesema watakaobainika kuhusika na madudu yaliyomo katika taarifa za kamati maalum za Bunge zilizoundwa kuchanguza masuala ya gesi asilia na uvuvi wa bahari kuu, watachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.

“Kuna watuhumiwa wawili wametajwa, vyombo vya dola vinatakiwa kuchukua hatua kwa wale walioghushi lesini za uvuvi,” amesema Mbarawa leo Juni 2, 2018 katika hafla ya kamati hizo zilizoundwa na Spika Job Ndugai, kukabidhi taarifa zake za uchunguzi kuhusu maeneo hayo mawili iliyofanyika viwanja vya Bunge mjini Dodoma

Mbarawa ambaye amemuwakilisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema, “Tumeyasikia mengi, Watanzania wamesikia mengi kuhusu ripoti hizi. Tutasoma ripoti hizi neno kwa neno, mstari kwa mstari na kipengele kwa kipengele. Niwahakikishe Bunge na Watanzania kwamba mapendekezo tutayatekeleza kwa haraka.”

“Kuna shida katika mikataba hasa gesi asilia. Utasikia kuna kasoro katika mikataba na Serikali ya Awamu ya Tano tumelisikia na tumejipanga na tutafanyia kazi. Kama ambavyo ripoti zimeeleza, wale ambao walihusika tutafanya uchunguzi na sheria itachukua mkono wake.”

Amesema katika sekta ya uvuvi kuna shida ya sera, kanuni ,sheria na kuahidi kuzifanyia kazi ili uvuvi uwe na maslahi kwa Taifa.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: