Mkuu wa shule ya Ufundi Mtwara Paul Kaji amepongeza serikali ya awamu ya tano kwa kuboresha miundombinu ya shule hiyo na hivyo kuondoa kabisa changamoto mbalimbali zilizojuwa kikwazo kwa wanafunzi na walimu shuleni hapo.

==>> Unaweza Kuidownload << kwa Kubofya Hapa>>

Kaji ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na timu ya wanahabari waliofika shuleni hapo kwa lengo la kuangalia ukarabati wa miundombinu ya shule hiyo ambapo zaidi ya bilioni moja imetumika kukarabati vyumba vya madarsa, ofisi za walimu, mabweni, Bwalo la chakula, sehemu za kuandalia chakula( majiko), kukarabati njia Maalumu za wanafunzi wenye ulemavu, kurejesha miundombinu ya umeme na Maji katika hali ya kawaida.

Pia baadhi ya wanafunzi waliohojiwa wameelezea kufurahishwa na ukarabati huo na hivyo kuwafanya wako Fundi katika mazingira mazuri.
“ Tunaishukuru serikali kwa kutuboreshea miundombinu ya shule siyo tu shule yetu imependeza Bali hata sisi tunaiwezo wa kusoma muda wowote kwa kuwa umeme upo, tunawasilisha feni na hivyo tunaahidi tutasoma kwa bidii ili tufaulu vizuri” anasema David Andrew mmoja wa wanafunzi wa kidato Cha pili katika shule hiyo ambaye anasomea fani ya ujenzi.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mbawala Ali Haroun amesema licha ya kujenga madarasa mapya lakini jambo ambalo limeleta heshima kwao ni ujenzi wa matundu ya vyoo.

Alisema katika fedha hizo wamejenga matundu ya vyoo 10 na kufanya jumla ya vyuo 16 na madarasa nane jambo ambalo limesaidia kuongeza wanafunzi na kila darasa kukaa wanafunzi kulingana na ukubwa wa darasa.

Hata hivyo aliongeza kuwa matundu ya vyoo yamewasaidia katika kuhakikisha walimu wanakaa mashuleni muda wote kuliko hapo zamani ambapo ilikuwa ni lazima kwenda kujisaidia majumbani mwao.

‘’Hapo awali kuliwa na shida kabisa kwani walimu walikuwa wanafika shuleni wakijisikia kubanwa na haja wanakimbilia nyumbani na kuwafanya kuchukua muda mwingi hadi wa vipindi ndipo wanarejea shuleni kwa ajili ya kuendelea na masomo,’’

‘’ Programu hii ni mkombozi kwetu kwani hata wanafunzi waliokuwa wakikaa katika madarasa kwa kubebana sasa wanakaa kwa nafasi na mpaka chumba kimoja kimebaki kwa kukosa wanafunzi,’’aliongeza mwalimu Ally.

Naye mwalimu,Isabela Mwambona alisema mradi huo umewarahisishia kazi kutokana na kufundisha kwa nafasi na hata kuwafikia wanafunzi  mmoja baada ya mwingine kwa ufundishaji.

Katika hatua nyingine programu ya Kusoma, Kuandika na  kuhesabu (KKK) imezaa matunda katika shule mbalimbali za Lindi na Mtwara.

Isabela  alisema tangu wapewe mafunzo ya kufundisha watoto kwa KKK kwa kutumia vitendo na michoro kwa sasa wamefanikiwa kupunguza idadi ya wasiojua kusoma na kuandika shuleni hapo.

Imetolewa na:

Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini

WIZARA YA ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIA

16/05/2018
Share To:

msumbanews

Post A Comment: