Unaikumbuka #Pogback? Hashtag maarufu sana Twitter wakati Paul Pogba akinunuliwa kwa dau la £89m kwenda United, Manchester walionesha umwamba wao wa pesa na dunia nzima ikajua kweli United wanataka kurudi juu.
Msimu wa kwanza EPL kwa Mfaransa huyu ukawa mgumu mno, maneno yakaanza. Wakasema Paul Pogba apewe msimu mwingine EPL ili azoee ligi hiyo kwa mara nyingine na msimu wenyewe ni huu.
Mwezi January Paul Pogba aliingia kwenye mzozo ambao haukuonekana mkubwa lakini inaonekana kama tatizo kwa Mourinho, hii ni baada ya majibizano katika mstari wa kuingilia uwanja wakati wa mchezo dhidi ya Tottenham.
Pogba ameshalia na Mourinho kuhusu nafasi anayochezeshwa akidai uhuru zaidi uwanjani, na wakati Kelvin De Bryune akiwa ametengeneza nafasi 103 katika EPL, Pogba ametengeneza nafasi 34 tu na yuko nafasi ya 31 katika watengeneza nafasi.
Hata katika wachezaji ambao wamepiga pasi nyingi zilizowafikia walengwa bado Pogba anaonekana kuyumba, amepiga pasi 1435 huku akiwa nafasi ya 18 na Granit Xhaka anayeongoza orodha ya wapiga pasi timilifu ana pasi 2711.
Kuna habari kwamba Jose Mourinho hana mpango na wachezaji walioboronga dhidi ya West Brom, hana mpango wa kuwapanga dhidi ya Tottenham na inadaiwa kwamba wengi ndio wataondoka.
Mourinho ameanza kuwaza kumpunguza Paul Pogba katika kikosi chake, na habari ni kwamba ni kati ya wachezaji ambao watawekwa sokoni dirisha lijalo la usajili, Mou ndio boss United na ndio anataka timu yake iweje kama amemchoka Pogba baasi ni wazi anakaribia kuuzwa.
Post A Comment: