
MWANANA
Hamisa Mobeto ameibua gumzo wakati wa utoaji wa tuzo za Sinema Zetu
baada ya kuamua kumtaja msanii maarufu Nassib Abdul a.k.a Diamond
Platnumz ndio amemvutia zaidi kwa wageni waliofika kwenye sherehe hizo
za utoaji tuzo.
Jina
la Mobeto si geni kwa Watanzania walio wengi na hasa wanaofuatilia
maisha ya mastaa wa kibongo na umaarufu wake uliongzeka zaidi baada ya
kubainika amezaa na Diamond.
Usiku
wa jana Mobeto alikuwa moja ya wageni waalikwa katika utoaji wa tuzo
hizo ambazo zimeandaliwa na Azam TV kupitia chaneli ya Sinema Zetu.Ndani
ya ukumbi huo alikuwepo na Diamond.
Wakati
mambo yakiendelea ukumbini hapo ndipo moja ya washehereshaji alipoamua
kumfuata Hamisa Mobeto na kisha kumuuliza ni nani ambaye anaona
amependeza ukumbini hapo kuliko mtu mwingine yeyote na anafurahia uwepo
wake.
Jibu
la Hamisa Mobeto bila kuchelewa akataja jina la Diamond.Wakati anaaza
kuulizwa Diamond alikuwa anasikilizia kwa umakini mkubwa na baada ya
kutajwa yeye akajikuta aking'ata meno kwa nguvu na kwa muda wa zaidi ya
dakika tatu akiwa ameshika kichwa chake.
Hata
hivyo ukumbini hapo wageni waalikwa walilipuka kwa shangwe kwa kupiga
kelele.Wakati Hamisa akimtaja Diamond, Wema Sepetu aliyekuwepo eneo hilo
yeye alionekana akiwa 'bize' na kuchati kwenye simu yake ingawa sura
yake ilionekana kutofurahia.
Ilipofika
muda wa kutoa zawadi kwa moja ya washindi wa tuzo hizo akaitwa tena
Diamond na Hamisa Mobeto wapande jukwaani kutoa tunzo.Hali hiyo
ikamfanya Diamond kukosa la kufanya.
Hivyo
akatumia nafasi hiyo kupongeza Azam TV kwa kuandaa tuzo hizo kwani
zimewakutanisha wasanii mbalimbali na hata yeye amepata nafasi ya
kukutana na mzazi mwenzie(Hamisa) na kufafanua hata mtoto wao akiona
atafurahia kuona wakiwa wawili jukwaani hapo.
Post A Comment: