Mzazi mwenzie na msanii Alikiba Devotha ambaye amezaa naye mtoto wa kiume anayefahamika zaidi kwa jina la Unju amefunguka mazito katika siku maalum ya msanii Alikiba ambaye anaoa leo April 19, 2018 na kuonyesha jinsi gani yeye ametoa baraka kwa Alikiba kuoa.
Mama Unju amesema kuwa yeye atahudhuria katika harusi hiyo ila anakwenda kama mama wa Alikiba na kudai kuwa msanii huyo amekuwa baba bora siku zote na kumtakia aendele hivyo hivyo hata baada ya kuoa.
"Leo ni siku yako maalum Kiande wangu, rafiki yangu na baba bora Alikiba, baba usiniangushe somo yako. Mungu akusimamie katika ndoa yako. Mimi leo naenda kama Mama K, ukawe mume bora na ujali familia zote, nenda mwanangu" alimalizia Mama Unju.
Ndoa ya msanii Alikiba inafanyika nchini Kenya katika mji wa Mombasa leo April 19, 2016 ambapo msanii huyo atachukua jiko lakini pia inategemewa kufanyika sherehe nyingine nchini Tanzania siku za karibuni ndani ya mwezi huu
Post A Comment: