Home
Kitaifa
RIPOTI: Taarifa za wabunge wa CCM zinaaminika kuliko za wabunge wa Upinzani
Leo Machi 29, 2018 Taasisi ya Twaweza imezindua ripoti yake ya
Utafiti wa Sauti za Wananchi awamu ya 25, ambapo umeonesha kuwa taarifa
zinazotolewa na wabunge wa vyama vya upinzani zinaaminika kwa watu
asilimia 12 pekee huku zile zinazotolewa na wabunge wa chama tawala cha
CCM zinaaminika kwa wananchi asilimia 26.Kwenye ripoti hiyo ya Twaweza imeonesha kuwa taarifa zinazotolewa na
Rais zinaaminika kwa asilimia 70 ya wananchi huku zinazotolewa na Makamu
wa Rais zikiaminika kwa asilimia 64.
Kwa maana nyingine, asilimia 16 ya wananchi hawaamini kabisa taarifa
zinazotolewa na wabunge wa upinzani huku asilimia 6 pekee ya wananchi
hawaamini taarifa zinazotolewa na wabunge wa CCM.
Aidha ripoti hiyo pia imeonesha kuwa taarifa zinazotolewa na
wanachama wa vyama vya upinzani zinaaminika kwa asilimia 9 ya wananchi
huku wanachama wa chama tawala cha CCM taarifa zao zikiaminika kwa
asilimia 27.
Kwa upande mwingine ripoti hiyo imeonesha kuwa taarifa zinazotolewa
na wenyeviti wa mitaa na vijiji zinaaminika kwa asilimia 30 ya wananchi.
Back To Top
Post A Comment: