Kamanda wa Polisi Kanda Maalum jijni Dar es salaam, Lazaro Mambosasa, ameelezea hatua inayoendelea kuchukuliwa juu ya askari polisi sita waliokuwa wameshikiliwa kutokana na kifo cha mwanafunzi wa NIT Akwilina Akwilin, aliyeuawa kwa risasi mapema mwaka huu

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam, Kamanda Mambosasa amesema polisi hao bado wapo kwenye uchunguzi kubaini ni nani anahusika, kwani mpaka sasa hakuna ushahidi wa moja kwa moja wa kuweza kumbaini.

“Wale walipokamatwa tulieleza bayana kwamba upelelezi unafanyika ili kujua ni nani ambaye ametenda kosa lile, bado suala la upelezi linaendelea.

"Yapo maelekezo yaliyotolewa ambayo tunaendelea kufuatilia ili kuja kubaini, ikumbukwe silaha moja ambayo haijajulikana ni ipi ndio ilikwenda ikamgusa Akwilina, lakini kama ulivyojua askari walikuwa ni wengi lakini pia kulikuwa hakuna ushahidi kwamba yupi aliyekuwa ametenda hivyo, kwa hiyo uchunguzi bado unaendelea”, amesema Kamnda Mambosasa.

Ikumbukwe kwamba mnamo Februari 17, mwaka huu, mwanafuzi wa chuo cha usafirishaji jijini Dar es salaam Akwilina Akwilini alifariki dunia baada ya kupigwa risasi ambayo inaaminika ilitoka kwa mmoja wa askari waliokuwa wakitawanya maandamano ya wafuasi wa chadema, huku yeye akiwa kwenye daladala akipita njia.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: