Msanii wa BongoFleva anayefanya vizuri ndani na mipaka ya nje ya Tanzania, Aslay amekanusha tetesi za kujihusisha kutoka kimapenzi na Vicky Kamata na kudai mwanamama huyo yupo kama mshauri wa kazi zake nasio vinginevyo.
Aslay ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza katika kipindi cha 'FRIDAY NIGHT LIVE' (FNL) inayorushwa na tinga namba moja kwa vijana baada ya kuwepo kwa tetesi zilizokuwa zinadai msanii huyo kujihusisha kimapenzi na mwanamama huyo ambae amemzidi umri mara dufu.
"Vicky Kamata nakumbuka nilimfuata kuomba ushauri kipindi Yamoto Band ilikuwa imeanza kuyumba, alikuwa na nia ya kutaka kunisaidia lakini baadae na yeye alibanwa na kazi zake kwa hiyo akashindwa muziki na vitu vingine japokuwa aliniambia kitu gani nifanye katika kazi zangu. Vicky kwangu ni kama mshauri au mama yangu kabisa", amesema Aslay.
Pamoja na hayo, Aslay ameendelea kwa kusema "sio kitu kizuri kabisa yule ni mtu ameolewa ana mumewe na anawatoto wakubwa kama mimi. Sijawahi kukaa kufikiria kitu kama hicho katika maisha yangu".
Kwa upande mwingine, Aslay amewataka mashabiki na wapenzi wa muziki wake wakae mkao wa kula kwa  ngoma mpya ambayo atakuwa yeye binafsi muda wowote kutoka sasa.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: