Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imewapiga marufuku wananchi wa Tanzania kujichukulia sheria za barabarani mkononi kwa kuweka matuta katika barabara bila ya kuvishirikisha vyombo husika kwa madai kitendo hicho kinasababisha ajali.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa wizara hiyo Atashata Nditie katika mkutano wa 10 kikao cha tano cha Bunge kinachoendelea mjini Dodoma wakati alipokuwa akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Mbunge Joseph Kizito Mhagama alilotaka kufahamu serikali ina mpango gani wa kumuwajibisha Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) pale ambapo sababu ya ajali inaonekana ni kutotekeleza utaratibu wa wakala huyo.
"Ni kweli kuna ubovu wa barabara na serikali imekuwa ikiendelea kufanya jitihada za kurekebisha ubovu huo na kuhakikisha kwamba barabara zetu kuu na zile za mikoa zinapitika kila wakati", amesema Nditie.
Aidha, Naibu Waziri huyo amedai kumekuwa na tabia ya hivi karibunui kwa baadhi ya wananchi kujichukulia maamuzi mkononi kuweka matuta bila ya kuambiwa.
"Kitendo hicho kimekuwa chanzo kimoja wapo cha ajali mbalimbali kwa sababu wanapoweka matuta bila ya kuwashauri au bila ya kuwaambia (TANROADS) inamaana yale matuta yanakuwa hayana alama na magari yanapokuja yanafika na kuparamia yale matuta na kusababisha ajali",amesisitiza Nditie.
Pamoja na hayo, Nditie ameendelea kwa kusema "niwashauri watanzania wasiweke matuta barabarani bila ya kutoa taarifa kwa vyombo vinavyo husika na barabara ili iwekwe alama ya kuwaoensha madereva kwamba kuna tuta mbele wanapokwenda. Lakini nimwambie tu Mbunge Mhagama kwamba Tanroads wanajitahidi sana kufanya kazi zao kwa uaminifu na umakini wa hali ya juu wakizangatia usalama wa watanzania".
Kwa upand mwingine, leo Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Dkt. Adelardus Kilangi ameapishwa rasmi kiapo cha uaminifu Bungeni ili aweze kuitumikia serikali pamoja na wananchi wake kiujumla.
Share To:

Post A Comment: