Msanii wa muziki na filamu nchini, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, ameweka wazi kuwa siku za hivi karibuni anaweza kukabidhiwa gari yake kutoka kwa Harmonize baada ya kumwahidi siku ya harusi yake.
Mrembo huyo aliahidiwa gari aina ya Noah, hivyo inadaiwa kwamba gari hiyo tayari imenunuliwa na kilichobaki ni makabidhiano mbele ya vyombo vya habari.
“Ni kweli Harmonize ameniambia gari lipo tayari na kilichobaki ni kukabidhiana, mambo yakiwekwa wazi kwenye vyombo vya habari yanatakiwa kuishia huko huko, kwa kuwa watu tayari wameanza kusema kuwa nimetapeliwa, lakini ukweli ni kwamba Harmonize hashindwi kitu,” alisema Shilole.
Harmonize aliahidi gari lenye thamani ya Sh milioni 9 ili liwasaidie wawili hao katika shughuli zao za biashara.
Share To:

Post A Comment: