Mbunge wa Jimbo la Mikumi Joseph Haule 'Prof Jay' amefunguka na kusema kuwa leo Februari 24, 2018 kuna watu watatu ambao ni majeruhi wa kupigwa risasi lakini mpaka sasa hawajapatiwa matibabu na wanashikiliwa na jeshi la polisi. 
Prof Jay amesema kuwa mwanachama mmoja wa CHADEMA ambaye amemtaja kwa jina la Aida Ulomi ameamua kugoma kula ili apatiwe haki yake ya msingi kwani hakufikishwa mahakamani kama ambavyo sheria zinataka iwe. 
"Leo ni siku ya 9, Tangu Kamanda mwenzetu Aida Ulomi apigwe risasi ya mguu, polisi bado wanamshikilia kituo cha Oysterbay na wengine kadhaa bado wanashikiliwa kwenye vituo mbalimbali, hajapelekwa mahakamani, hana matibabu yeyote na amegoma kula, twendeni tukamwone na kumsaidia" alisema Prof Jay 
Mbali na huyo pia Mbunge wa jimbo la Tarime vijijini John Heche amewataja watu wengine ambao nao walipigwa risasi Februari 16, 2018 wakati jeshi la polisi likiwatawanya wanachama wa CHADEMA ambao walikuwa wakiandamana kwenda kwa Mkurugenzi wa uchaguzi jimbo la Kinondoni kudai barua za utambulisho wa mawakala wao. 
"Mpaka sasa ni watu watatu wanashikiliwa na jeshi la Polisi katika kituo cha osterbay Polisi. Wote ni majeruhi Wa risasi wanauguza vidonda na haki yao ya kupata matibabu imevunjwa. Hapo ni Aida Olomi...Kigamboni, Issack lomanus Ngaga....Kibaha, Erick John.... Kinondoni. Jana siku nzima wako kwenye vikao na bado wanatupiana mpira, kila ngazi inasubiria maelekezo kutoka juu. Ni uvunjifu Wa Sheria za nchi na taratibu za haki za binadamu" Alisema Heche 
Share To:

msumbanews

Post A Comment: