Kikosi cha timu ya Simba.

KOCHA msaidizi wa Simba Mrundi, Masoud Djuma amekiri ugumu wa mechi yao ya leo dhidi ya Azam FC, huku akitaja mbinu za ushindi katika mchezo huo ni kuanza kukabia kwenye lango la wapinzani.

Kauli hiyo, aliitoa hivi karibuni mara baada ya mechi dhidi ya Ruvu Shooting kumalizika iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam iliyomalizika kwa Simba kushinda mabao 3-0.

Simba wanaoongoza ligi wakiwa na pointi 38, leo itashuka kwenye Uwanja wa Taifa, Dar kuwavaa Azam waliokuwa katika nafasi ya pili wakiwa na pointi 33 mechi ambayo kila timu inahitaji ushindi ili ijiwekee mazingira mazuri ya ubingwa wa ligi kuu.

Akizungumza namwandishi wetu, Djuma alisema ; “Kitu cha kwanza tutakachokifanya katika mechi hiyo na Azam ni kutowaruhusu kufika na kucheza kwenye lango letu kwa hofu ya kufanyika makosa, hivyo hatutaki golini kwetu mpira ukae.” 

“Kingine, tutaingia uwanjani hapo kwa kuanza kuwakabia Azam kwa kuanzia golini kwao kwa maana ya viungo, mawinga na washambuliaji muda wote wanatakiwa kuwepo kwenye goli la wapinzani wetu. “Kama unavyofahamu, mpira ni mchezo wa makosa hivyo tunataka kutumia makosa yao katika mechi hiyo kuwafunga, “ alisema Djuma.
Share To:

Post A Comment: