Na:Netho Ndilito
.............................................
Nichukue Fursa hii adhimu sana,Kuupongeza Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Arusha,Chini ya Uongozi mahili Na adirifu wa Mwenyekiti Mh.SAITOT ZELOTH,Katibu Goha,Viongozi wa Wilaya zote,wajumbe wote na Vijana wa Mkoa wa Arusha.

Hongereni sana Sana,kwa kuendeleea kuimarisha jumuia hii Na kiunganisho kikubwa kati ya wananchi,Wanachama Na Vijana wa Arusha.Nafahamu Kazi Kubwa inayofanywa na viongozi wetu wa Jumuia,katika ngazi zote,Kazi yenu ni heshima kuu MBELE za Mungu.

Ninafikiri kipindi cha Uchaguzi kimeisha,Kila jumuia ndani ya chama cha Mapinduzi imeendelea kukamilisha safu yake ya uongozi kwa mujibu wa kanuni,Taratibu na miongozo ya chama cha Mapinduzi.Kwa Mara nyingine nimpongeze sana Rafiki yangu ,Ndugu yangu Na shemeji yangu OMARI Lomato kwa kuchaguliwa Na wajumbe kuwa Katibu Hamasa Na Msemaji Mkuu wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Arusha.Hongera sana.Juhudi zako,Uadirifu wako, Upendo wako ndio umefanikisha kutimiza ndoto yako ya Muda Mrefu.Sisi Vijana wa Arusha tunakuahidi ushirikiano Mkubwa ambao matokeo yake ni kuyarudisha Majimbo yote yaliyoko mikononi mwa Maharamia wa kisiasa Mkoani Arusha Na Tanzania kwa Ujumla.

Hongera za pekee kwa akina mama zetu (UWT-Arusha)kwa kasi Kubwa Na nzuri mliyoanza nayo.Juhudi hizo ni kwa maslahi mapana ya chama,Jumuia na wanachama wa CCM.Tunawapongeza sana viongozi wa Jumuia ya Akina wanawake Mkoa wa kwa kusafisha Jumuia hiyo iliyokuwa imeundwa kama Taasisi binafsi ya watu wachache.Tumesikia Ubadhilifu Mkubwa Na wakusikitisha mnaoendelea kugundua.

Pongezi za Pekee kwa Mh.Mwenyekiti (Mzee wa Boma)Mwenyekiti CCM Mkoa wa Arusha Mh.SANARE.Hakika Arusha tumepata watu Na viongozi Makini sana,Wazalendo,wachapakazi ambao hakika watakivusha chama kutoka kifungoni kilipokuwepo Awali.Sasa ni mwisho kwa wasaliti,Wanafiki,Na wanaotumia mgongo wa chama kwa Maslahi yao binafsi.Hongera sana Mh.Katibu Mkoa wa Arusha Mh.MPANDA kwa Kazi nzuri sana.Nafikiri moja ya Mikoa uliyokuta CCM haiko imara ni Mkoa wa Arusha.Lakini Ujio wako umetusaidia sana sana kuimarisha chama Na kukifanya chenye nguvu sawa Na mataifa ya G8.Mh.Mpanda Mungu atalipa Kazi yako.

Niwapongeze pia viongozi wetu wa Serikali kwa Usirikiano mzuri waliotupa kipindi chote hiki.Wamekuwa Wasikivu kwa Chama ambacho kwayo wanatekeleza ilani ya CCM.Hongera sana Mkuu wa Mkoa wetu Mh.Gambo,Wakuu wa Wilaya wote,wakurugenzi Na Majeshi yetu kwa Kazi nzuri ya kutekeleza Ilani ya chama Cha Mapinduzi.

Sisi Vijana wa Arusha Na Wananchi wa Arusha Tunaomba Mtupelekee Na mkawe wasemaji wa changamoto zetu kwa Mh.Rais Dr.JPM Ikulu Dodoma au Dar es Salaam Na Sio Monduli Ikulu ya Chadema.


Mungu Awabariki Sana sana.

Netho Ndilito
(Hard Working & God Fearing Servant)
Share To:

msumbanews

Post A Comment: