MSANII wa Bongo Movie na Mtangazaji maarufu nchini, Faiza Ally amefunguka kuwa ikibidi ataandamana ili baba mtoto wake, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ apate haki yake baada ya kuwekwa mahabusu jana Jumanne, Januari 17, 2017 kwa kosa la kutoa maneno ya uchochezi.

Faiza ambaye amezaa na mbunge huyo mtoto mmoja, Sasha Desderia amefunguka kupitia akaunti yake ya Instagram akisema kuwa yeye na Sugu walitofautiana kuhusu mambo ya mapenzi tu, na hayo mambo yalishaisha hivyo anamuombea atoke akiwa salama.

Faiza ameandika
Just to let you know guys: kamwe sitaweza hata siku moja kufurahia matatizo ya baba Sasha kufurahia matatizo za baba Sasha hata ikibidi kuandamana apate haki yake ningefanya hivyo!

Matatizo yangu na yeye ni mapenzi tu na si vinginevyo na yaliisha! Mwisho wa siku ni baba wa mwanangu na wanapendana sana na mwanae wamefanana mpaka harufu zao kila ninapomuona namuona baba yake na nikifanya ubaya ntakuwa namfanyia mwanangu …
All I wish Sasha na baba yake wawe hai, wawe na furaha siku moja niwaone wako pamoja happy and success. So kama mnahisi nafurahia mpo wrong na kwa kifupi nimetafutwa na watu wengi, wa siasa na wanamuziki ili nimchafue au nishirikiane nao lakini sijawahi kuwapa nafasi.

Nikiwasha MOTO wangu ni wa sababu zangu binafsi na siyo kutumiwa and by the way amelipa ada ya Sasha and hope in future atakuwa baba bora zaidi kama alivyo mwanzo. Na ninamuombea heri Mungu amfanyie wepesi na amuonyeshe njia pasipo kuwa na njia!” ameandika Faiza.


Sugu akipelekwa mahabusu.
Sugu na Mratibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya jana Januari 16 kusomewa mashtaka yanayowakabili kisha kupelekwa mahabusu ya Gereza la Ruanda baada ya Wakili wa Serikali, Joseph Pande kuiomba mahakama kuzuia dhamana kutokana na usalama wa washtakiwa kutokana na kosa walililotenda.

Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite alikubaliana na ombi hilo ambapo aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 19, mwaka huu atakapotoa uamuzi wa dhamana.
Washtakiwa hao wanadaiwa kufanya uchochezi kwa kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli, Desemba 30, mwaka jana akiwa katika viwanja vya mikutano vya Shule ya Msingi Mwenge iliyopo jijini Mbeya ambapo Sugu anadaiwa kutamka kuwa rais ni muuaji.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: