Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limetoa ufafanuzi juu ya maamuzi ya mahakama kuhusu wabunge 8 wa CUF ambao walivuliwa uanachama na kupoteza sifa ya kuwa wabunge na kusema katika maamuzi ya mahakama hakuna sehemu iyosema watu hao warejeshewe Ubunge.
Aidha, katika taarifa iliyotolewa na Katibu wa Bunge imesema kuwa, wamekuwa wakiona kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari taarifa mbalimbali zikisema kuwa wabunge waliovuliwa uanachama na CUF wanatakiwa kurudishiwa ubunge wao.
Hata hivyo, taarifa hiyo imeongeza kuwa hakuna jambo la namna hiyo kwa kuwa nafasi zao tayari zilishajazwa na Tume ya Uchaguzi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment:

Back To Top