Msanii wa muziki wa bongo fleva ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Seduce me' Alikiba ameamua kuachia video ya wimbo wake wa zamani ambao ulivuja kama zawadi kwa mashabiki wake katika siku yake ya kuzaliwa.

Alikiba ambaye jana alikuwa anasherehekea kumbukumbu ya mwaka wa kuzaliwa aliamua kuachia video ya wimbo wa 'Maumivu Per Day' kama njia ya kusherekea siku hiyo na mashabiki zake.

"Nashukuru sana watu ambao wamenitakia kheri katika siku yangu ya kuzaliwa, nimejaliwa, kupendelewa na kupendwa pia nashukuru sana kwa jambo hilo, nawapenda wote na nitafanya kazi kwa nguvu zote kuwafanya mjivunie uwepo wangu. 

"Maumivu Per Day ni kati ya nyimbo zangu za zamani zinazopendwa nimeamua kuitoa japo siyo rasmi ili kusherehekea kumbukumbu ya siku yangu ya kuzaliwa na mashabiki zangu" alisema Alikiba


Share To:

msumbanews

Post A Comment: