Wakili wa Mahakama Kuu nchini, Ndg. Alberto Msando, amekana kumsaliti rafiki yake wa karibu na wa siku nyingi na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe mara baada ya kuhama chama cha Act Wazalendo na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).
“Mimi sijamsaliti Zitto Kabwe, niko tayari kupambana naye kwenye ulimwengu wa siasa, hatujaanza kupingana leo, nakumbuka alitaka kunipindua wakati tukiwa Chuo Kikuu mimi nikiwa spika wa Bunge la wanafunzi yeye akiwa waziri mkuu lakini baadae tulirudi na kufanya kazi katika serikali moja. Nikiri kwamba sijazungumza na Zitto toka nimehama Act wazalendo wala sikumpa taarifa juu ya mimi kuhama” amesema Msando wakati akihojiwa na Kituo cha Utangazaji cha Clouds leo asubuhi.
Alisema, yeye hana tatizo na Zitto, yeye ndo alimtambulisha kwenye ulimwengu wa sias.
“Hata nilipotoka Chadema nilikaa mwaka mzima na Mheshimiwa Mbowe lakini baadae tulizungumza na maisha yakaendelea, Siasa sio uadui,” alisema Mwanasheria huyo.
Tembelea mtandao wa darmpya.com kupata habari kila zinapotokea
Post A Comment: