Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro


Habari kutoka wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga zinaarifu kuwa vifaa vinavyotumika katika zoezi la kuhakiki vyeti kwa watumishi wa umma sambamba na kuandikisha vitambulisho vya taifa (NIDA) vimepotea katika mazingira ya kutatanisha katika jengo la ofisi ya halmashauri ya wilaya ya Kishapu.




Inaelezwa kuwa vifaa vinavyodaiwa kuibiwa na watu wasiojulikana ni kamera mbili na viegesho vyake (stand mbili) 



Akizungumza na Malunde1 blog kwa njia ya simu Mkuu wa wilaya ya Kishapu ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo Nyabaganga Talaba amesema vifaa hivyo vimebainika kupotea leo Jumatatu Oktoba 10,2016 asubuhi. 


Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Stephen Magoigaamesema vifaa vilivyopotea ni kamera mbili na viegesha vyake vilivyokuwa vimehifadhiwa kwenye ofisi ya halmashauri yake kwa ajili ya kupigia picha za NIDA. 


Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliroameiambia Malunde1 blog kuwa uchunguzi juu ya tukio unaendelea. 


TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA   HABARI. 
TUKIO LA KUIBWA KWA CAMERA 2 ZAUINDIKISHAJI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA (W) KISHAPU.
TAREHE 10.10.2016  SAA 08:00  KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA KISHAPU KATA, NA TARAFA YA KISHAPU ZONE 13 WILAYA YA KISHAPU MKOA WA SHINYANGA SOFIA D/O DIDAS LESHABARI, MIAKA 30, MMASAI, REGISTRATION OFFICER ONE  WA NIDA, MKAZI WA DAR-ES-SALAAM, ALIBAINI KUWA OFISI ILIYOKUWA INATUMIKA KATIKA ZOEZI LA UANDIKISHAJI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA KWA WATUMISHI WA UMMA KATIKA JENGO LA HALMASHAURI YA WILAYA YA KISHAPU GHOROFA YA KWANZA CHUMBA NAMBA 46 ILIVUNJWA / FUNGULIWA (TECHNICAL BREAKING) NA KUIBWA KAMERA MBILI AINA YA CANON NA STENDI ZA KAMERA MBILI AMBAZO ZILIKUWA KWENYE MASHINE MBILI ZA BVR ZENYE NAMBA TZNID 01546 NA TZNID 01559 ZENYE THAMANI YA TSH 6,000,000/= MALI YA SHIRIKA LA NIDA . WEZI/ MTU/WATU WALIOHUSIKA  BADO HAWAJAFAHAMIKA.

 MBINU ILIYOTUMIKA KUTENDA KOSA HILO NI KUFUNGUA MLANGO KWA KUTUMIA MASTER KEY. 

UPELELEZI UNAFANYWA ILI WOTE WALIOHUSIKA WAFIKISHWE MBELE YA MAHAKAMA.WATU WATATU WANAHOJIWA / SHIKILIWA NA POLISI KUHUSIANA  NA TUKIO HILO . RPC SHINYANGA.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: