Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anasema kuwa timu yake ''haikubabaika'' baada ya kufungwa bao moja katika dakika ya kwanza ya kombe la vilabu bingwa mjini Paris kabla ya kusawazisha na kupata droo ya 1-1.


Edinson Cavani aliwaweka PSG mbele baada ya sekunde 42 pekee na alikuwa na nafasi ya kufunga mabao matatu kufikia muda wa mapumziko.
Sanchez alifunga bao kwa kutumia vyema mpira uliodunda baada ya Arsenal kupata kombora la kwanza kabisa la kulenga goli.
Nyota wa Arsenal Olivier Giroud na Marco Verratti wa PSG walioneshwa kadi nyekundu.
Giroud alikuwa ameingizwa kama nguvu mpya na akajipatia kadi mbili za manjano katika dakika 27, ya pili ikitokana na kisa ambapo alikaripiana na Mwitaliano Verratti ambaye pia alipewa kadi ya pili ya njano.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: