MAWAZIRI wa nchi wanachama wa Jumuiyaa ya Afrika Mashariki wamekutana jijini Arusha,yalipo makao makuu ya Jumuiya hiyo ili  kuhitimisha mkutano wa Chakula na Usalama wa Chakula kwa nchi hizo.


Lengo la mkutano huo ni kuendelea kuimarisha na kutengeneza sera nzuri pamoja na sheria ambazo zitazisaidia nchi hizo kufanya kazi pamoja bila kuwa na migongano na kuwawezesha wananchi kunufaika na rasilimali zilizopo na kupata tija.

Katika mkutano huo ambao nchi ya Kenya ndio mwenyekiti kupitia kwa Waziri wa Kilimo,Ufugaji,Wanyama,Samaki,Vyama vya Ushirika na Uchumi Samawati  ambapo aliwakilishwa na mheshimiwa Lawrence Umuhaka.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi kwa Upande wa Tanzania Mh.Mashimba Ndaki ambaye ni moja ya mawaziri waliohudhuria kutoka Tanzania alisema kuwa mkutano huo wa mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni muhimu kwa kuwa una lengo la kuboresha sera za Uvuvi,Mifugo na Kilimo kwa nchi wanachama ili ziweze kuleta faida kwa nchi hizo.

Mh.Ndaki alisema kuwa wameangazia maeneo mengi ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa sera ya Mifugo ya Afrika Mashariki ili iendane na nchi zinazounda Jumuiya ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa kunakuwepo na sheria nzuri,na muelekeo mzuri katika sekta ya Mifugo na Uvuvi.

"Ndugu zangu Leo tumejadili mengi moja wapo ni Uboreshaji wa sera ambazo zitazisaidia kupata sheria nzuri ili tufanye kazi pamoja na kwa manufaa ya wananchi wetu,Pia Kuna Jambo moja ambalo limezungumzwa na linatarajiwa kupelekwa kwenye bunge la EAC na Mbunge mmoja kuwa kuwepo kwa sheria itakayoruhusu mifugo kutoka nchi moja kwenda nyingine bila kikwazo chochote kufuata malisho ikiwa hiyo nchi itakuwa inakabiliwa na malisho japo hili hatujafikia muafaka ni Pana Sana"Alisema Mashimba.

Aidha katika sekta hiyo ya Mifugo alisema kuwa swala la Usafirishaji Mizigo ya Mifugo kwa nchi za EAC,limejadiliwa na kinachofanyika sasa ni ufuatiliaji wa kina ambao utahitajika ili kuweza kuwekwa sawa na kuhakikisha linafikia mwisho na halileti mkanganyiko kwa wananchi.


Hata hivyo waziri Ndaki alisema kuwa nchi hizo zimekubalina kutunza rasilimali za Uvuvi ili ziweze kunufaisha  vizazi na vizazi kwa kuwa Eneo hilo ni muhimu Sana kwa nchi hizo.


"Tumekubaliana kwa Pamoja pia kuwa na taarifa moja ambayo itawezesha nchi zetu hizi kutoa taarifa zake na Kisha kuwepo na moja ambayo hatukuwa na utaratibu huo kabisa, badala yake tumekuwa tukitoa tarifa za Uvuvi ambao unafanyika katika ziwa Victoria tu wakati kuna bahari kama Kenya,Tanzania kuna ziwa Tanganyika nyasa na Mengineyo kwahiyo hili tutaboresha"Alisisitiza Mh.Ndaki

Nae naibu Waziri wa Kilimo Ufugaji Wanyama Samaki Vyama vya Ushirika na Uchumi Sanawati kutoka Kenya Lawrence Umuhaka alisema kuwa mkutano huo wa mawaziri ulitanguliwa na mkutano wa Wataalamu kutoka nchi za EAC, Makatibu wakuu na mawaziri ambao ndio watendaji wamehitimisha kwa kuangalia namna Bora ya kuresha sera mbalimbali zikiwemo za Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa lengo la Kuwezeshana nchi kushirikiana vizuri.


Mh.Lawarence alisema kuwa swala la Afya ya Mifugo limejadiliwa kwa mapana ili Kutafuta mbinu ya kukabili changamoto zilizopo za Magonjwa ya Mifugo ili kuondoa vikwazo na kuja na mkakati wa pamoja ambao utaisaidia jamii nzima na kuwawezesha wananchi kunufaika na Mifugo Yao.

Nchi zilizoshiriki mkutano huo ni Pamoja na Kenya, Burundi,Tanzania huku nchi za Rwanda,Sudani kusini na Uganda zikishiriki kwa nchi ya mtandao ambao sekta hizo muhimu za Kilimo Mifugo na Uvuvi zenye sera ya Pamoja ya EAC zikiendelea kuboreshwa ili kueleta tija kwa Wananchi wa Jumuiya hiyo na kuwawezesha kunufaika kiuchumi kwa kufanya kazi katika mazingira wezeshi na mazuri yasiyo na vikwazo.





Share To:

Post A Comment: