Afisa Udhibiti Ubora, Mhandisi Emmanuel Shilinde, akiwaonesha wanafunzi wa shule ya msingi Chato A na B wilayani Chato, alama ya ubora ya TBS ili waweze kuikumbuka wakati wanapotumwa kwenda kununua bidhaa zilizozalishwa nchini. Kupata alama ya ubora kwa wajasiriamali wadogo ni bure kabisa.

Afisa udhibiti ubora, Mhandisi Emmanuel Shilinde (TBS) akitoa elimu ya masuala ya viwango kwa baadhi ya wananchi wa eneo la Muganza, wilayani Chato mkoa wa Geita.

Mhandisi Emmanuel Shilinde (TBS) akiwahamasisha wafanyabiashara wa Chato Kati - Geita kusajili madukani ya chakula na vipodozi ili kuepuka usumbufu.

Wanafunzi wa shule ya sekondari Chato, wilayani Chato- Geita wakisikiliza kwa makini elimu ya viwango kutoka kwa maafisa wa TBS ili wawe mabalozi wazuri wa masuala ya viwango katika jamii zao.


TBS imeendelea kutoa elimu ya alama hya ubora wa bidhaa kwa wananchi Wilayani Chato ambapo wametembelea katika shule mbalimbali za wilaya hiyo na kuwapatia elimu ili waweze kufahamu bidhaa ambazo zimethibitishwa na shirika la hilo.

Lengo la utoaji elimu hiyo kwa shule ni kuwafanya wanafunzi kuwa mabalozi wazuri wa shirika hilo kuhusu alama za ubora kwenye bidhaa ili kuweza kumlinda mlaji au mtumiaji wa bidhaa.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: