Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Tulia Ackson ameshiriki Mkutano wa 65 wa Umoja wa Mataifa wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani (65th Session of the Commission on the Status of Women - CSW65) ambao umeanza leo tarehe 15 hadi 26 Machi 2021 New York, Marekani. 


Katika mkutano huo ulioandaliwa na Ubalozi wa Qatar ukishirikiana na Tanzania, Japan, India, Sweden na ESCWA. Mada kuu ya mkutano huu ikiwa kuimarisha ushiriki wa wanawake kwenye siasa ili kufikia malengo endelevu ya maendeleo, (Enhancing Women’s Political Participation to achieve the SDG’s and Build Back Better)


Akichangia kwenye mkutano huo kwa njia ya mtandao, pamoja na mambo mengine, Dr. Tulia ameeleza jinsi ambavyo Tanzania imeweza kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi katika nyanja mbalimbali ikiwemo upande wa kisiasa huku akizitaka nchi nyingine dunini kuiga mfano huo wa kutoka Tanzania.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: