Tuesday, 4 February 2020

CCM ILALA KUZINDUA USIKILIZAJI WA KERO ZA KISHERIA


Okye
Na Heri Shaaban

CHAMA cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala February 4 inazindua utaratibu wa kusikiliza kero za kisheria kupitia wana sheria wana  CCM.

Akizungumza na waandishi wa habari CCM wilaya ya Ilala Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Ubaya Chuma alisema utaratibu wa kusikiliza kesi hizo ni endelevu kwa wiki Mara mbili.
H
" Chama cha Mapinduzi CCM Ilala tunanzindua utaratibu wa kusikiliza  kero za kisheria zinazowahusu wana CCM peke yake na zitatatuliwa na wanasheria wana CCM " alisema Chuma .

 Alisema wilaya ya Ilala ni kubwa   wana CCM wengi wanakuwa na kesi mbalimbali za kisheria wanashindwa waende wapi kwa wakati huo kwa ajili ya kupata ushauri.

Chuma alisema CCM  Ilala imeamua   kuweka utaratibu huo kwa ajili ya kuwaondolea adha wana CCM wa Ilala ambao wana kesi za kisheria hawajui wazipeleke wapi  ili ziweze kupata ushauri na utatuzi.

No comments:

Post a comment