NA HERI SHAABAN
KAMATI ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Dar es salaam wameipongeza miradi ya Maendeleo ya Rais ambayo inatekelezwa Halmashauri ya Ilala.

Pongezi hizo zilizotolewa na Katibu wa CCM mkoa huo Zakaria Mwansasu, wakati wa ziara wilayani Ilala kuangalia miradi ya maendeleo ikiwemo miradi mkakati ya soko la kisasa Kisutu na mradi wa Machinjio ya Vingunguti.

Akitoa pongezi hizo Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Dar es salaam Zakaria Mwansasu alisema kama viongozi wa kamati ya siasa ya mkoa wamefurahishwa na miradi hiyo mkakati iliyopo halmashauri ya Ilala fedha za ujenzi zimetumika kihalali.

" Mradi wa machinjio ya Vingunguti mzuri una faida kwa wananchi utaongeza ajira kwa watanzania naomba tupongeze juhudi za Rais John Magufuli  na kumuunga mkono  utekelezaji wa juhudi zake"alisema Mwansasu

Alisema Katika nchi yetu mradi wa Vingunguti ni wa kujivunia  fursa zitaongeka .

Katibu Mwansasu akielezea dhumuni la ziara hiyo alisema kukagua Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM katika wilaya ya Ilala utekekezaji wake wakati chama cha Mapinduzi kinavyoelekea kutimiza miaka 43 sambamba na ziara kuangalia chama kilivyotekeleza ilani.

Katika hatua nyingine Katibu Mwasasu ameagiza Meneja wa Shirika la Umeme Tanesco kuamisha nguzo za umeme zinachangia mradi huo kuchelesha ujenzi wake.

Ziara hiyo pia ilikagaua mradi wa soko la kisasa Kisutu, hospitali ya Wilaya Kivule, sekta ya elimu shule ya Msingi Gongolamboto, Shule ya Msingi Gurukwalala, na Sekondari ya Vingunguti.

Akiekezea upande wa sekta elimu alivyokagua ujenzi wa Shule ya Gurukwalala aliagiza ifatiliwe mipaka ya shule hiyo na kufanya utaratibu wa kumwamisha mwananchi mmoja ambaye nyumba yake  ipo eneo la shule.

Kwa upande wake Afisa Elimu Msingi Ilala Elizabeth Thomas alisema ujenzi wa shule hiyo utakamilika hivi karibuni ambapo katika shule hiyo yanajengwa madarasa 23,jengo la Utawala Ujenzi wa nyumba ya mwalimu, matundu kumi ya vyoo na mfumo wa maji safi na salaam.


 Naye Mkurugenzi wa halmashauri ya Ilala Jumanne Shauri alisema mradi huo wa Machinjio ya Vingunguti Wilayani Ilala ukikamilika utakuwa umeondoa umasikini watu 3000 watapata ajira kwa siku watu 300 watafanya kazi  ng'ombe 500 watachinjwa na Mbuzi 1000.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Ubaya Chuma amepongeza Wakuu wa Idara wa Halmashauri hiyo na Watumishi wake kwa kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo ambayo inatarajia kukamilika hivi karibuni.

Mwisho
Share To:

msumbanews

Post A Comment: