WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella wakioangalia maeneo mbalimbali ya mabwawa hayo 
 WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa kushoto akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe kulia katikati ni Mbunge wa Jimbo la Handeni mjini (CCM) Omari Kigoda kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella aliyevaa kofia na miwani 
 WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa katikati akiwa na Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini (CCM) Omari Kigoda kushoto na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Handeni William Makufwe
 WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa  katikati akisisitiza jambo kwa  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga wakati alipotembela eneo la mabwawa hayo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Handeni (CCM) Omari Kigoda 
 muonekano wa moja ya mabwawa ya maji wilayani Handeni
WAZIRI wa Maji Pro,Makame Mbarawa amelazimika kufanya ziara ya  wilayani Handeni Mkoani Tanga ili kuona namna ya kuweza kuwanusuru zaidi wananchi elfu 55 waliokumbwa na tatizo la kukosa huduma ya maji safi na salama kutokana na mabwawa 12 yaliyokuwa yakitumika kutoa huduma hiyo kuathirikawa na mvua zilizonyesha Mkoani hapa.

Mvua hizo ambazo zilisababisha athari kubwa ya kusomba mabwawa hayo ya maji na kupelekea wananchi hao kukosa maji wilayani humo jambo lililomlazimu Waziri huyo kuambatana na viongozi Mamlaka mbalimbali za maji ili kuweza kurudisha huduma hiyo na kuwanasuru wananchi hao na ukata wa maji.

Akizungumza mara baada ya kutembelea mabwawa hayo yaliyobomolewa na na mvua hizo, Waziri Mbarawa alisema kwamba hilo ni janga ambalo linaweza kutokea wakati wowote hivyo kupitia Mamlaka zilizopo watahakikisha mji huo unapata maji kwa kuunganisha na mradi wa maji wa htm Korogwe ambao utaleta maji Handeni ambapo kunatakiwa bomba la mita 300 wataalamu wataletwa ili kuweza kufanikisha suala hilo.

 “Leo Bomba litafika kwa sababu kuna miradi mingi inaendelea kwenye mamlaka zote nchini watatoa bomba haraka lije hapa na tuna timu ya wataalamu kutoka mikoa ya Moruwasa, Tanga Uwasa na Dawasa lakini bomba likifika haraka lifungwe kuondosha changamoto hiyo haraka “Alisema  

Waziri Mbarawa alisema kwamba wataalamu wanapaswa kufanya kazi kwa kipindi cha wiki moja ili huduma ya maji iweze kujerejea Wilayani hapa huku maeneo ya vijiji yaliyoathirika wataalamu wa bonde la mto Pangani wanatakiwa kuchimba visima harakaharaka na kwa kutumia gari lililopo  Wilayani Pangani namba 83 kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.

“Tunachokifanya hapa ni jambo la dharura hawa watu watakao kuwa na shughuli za uchimbaji wa visima natambua watu wa Tanga-Uwasa wapo hapa mtawapatia fedha kwa ajili ya shughuli hiyo na ianze mapema iwezekanavyo”Alisema Prof,Mbarawa.

Akizungumzia mipango ya muda mrefu alisema ili kuondoa tatizo hilo watahakikisha wanaona namna ya kujenga miundombinu imara ikiwemo kuongeza nguvu kwa lengo la kuweza kuyaangalia upya mabwawa yote yanakuwa salama zaidi ili zinaponyesha mvua zisiweze kuleta athari kama iliyojitokeza na kupelekea wananchi kukosa huduma hiyo muhimu.

“Lakini pia tutahakikisha tunayalinda mabwawa hayo kwasababu bwawa ni jambo kubwa sana na kama tusipifanya hivyo yanaweza kupasuka na kuleta athari kwa wananchi pia tutaangalia mipango yake ya kupitia na sisi wizara tutaongeza nguvu na utaratibu mpya kuweka ulinzi kwenye sehemu ya mipango yake ya kupitia kama yanaweza kupita na yanakuwa salama na wananchi waweze kuepukana na athari”Alisema

Akieleza namna walivyopambana na suala hilo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella alisema baada ya kuwepo kwa tatizo hilo  alikutana na Meneja wa Ruwasa Mkoa ambaye alieleza namna alivyoandika mapendekezo yake na na kuyawasilisha wizarani ambpo waziri huyo ulimuelekeza Naibu Kati bu Mkuu ufike eneo hilo na aweze kujionea hali halisi.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kwamba jambo hilo liliwapa faraja kubwa kutokana na kwamba serikali kuwakimbia wakati wa tatizo hilo ambalo lilikuwa limeshawavuka uwezo wao lakini kwa ujio wake wanamatuimani wanaweza kupata ufumbuzi wa mji huo kupata maji ya kutosha.

“Ninaishukuru wizara imefanya jambo kubwa muhimu kufanya kuhakikisha Handeni inapata maji ya kutosha ambayo miaka ya nyuma haikuwahi kupata na changamoto hiyo imepeleka kubomoka madaraja na barabara kwa maana presha ya maji ikawa kubwa hivyo niishukuru sana “Alisema RC Shigella.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: