Naibu waziri wa Wizara ya mifugo na uvuvi  Abdalla Ulega akimkabidhi kombe la ushindi mkurugenzi wa TAHA Jacqueline Mkindi Mara baada ya kushinda katika sherehe za wakulima Kanda ya kaskazini.
 Naibu waziri wa Wizara ya mifugo na uvuvi  Abdalla Ulega akihutubia wananchi wakati akifunga sherehe za maonyesho ya nanenane  Kanda ya kaskazini yaliofanyika jijini Arusha
bendi ya Polisi Moshi ikitumbuiza mbele ya mgeni rasmi wakati wa kilele cha maonyesho ya nanenane Kanda ya kaskazini yaliyofanyika njiro Themi jijini hapa.

Na Woinde Shizza ,Arusha

 Naibu waziri wa Wizara ya mifugo na uvuvi  Abdalla Ulega amesema kuwa Elimu  na ujuzi  Wa vitendo ipelekwe kwa wakulima wa vijijini pamoja na wafugaji ili kuwa na wafugaji wenye kufuga kisasa  na hatimaye kuchangia katika  kufikia  uchumi Wa viwanda kama kauli mbiu ya maonyesho ya mwaka huu ya nane nane inavyosema     Kilimo ,mifugo  na uvuvi kwa ukuaji Wa uchumi Wa nchi.

Naibu waziri Ameyasema hayo Leo wakati akifunga maonyesho ya 26 ya  kilimo na mifugo (nanenane )kwa Kanda ya kaskazini yalikuwa yakifanyika katika viwanja vya Themi Njiro ambapo alisema kuwa  kwakuzingatia kauli mbiu maarifa haya yaliotolewa katika maonyesho haya yasipoishia hapa  nchi yetu itajitosheleza  kwa chakula  na mifugo  na hatutakuwa na haja ya kuitaji chakula cha msaada bali tutakuwa na chakula cha kutosha .

Alibainisha kuwa tukichukuwa ujuzi huu tulioupa hapa tutapata mazao bora na mifugo ambapo tutauza mazao ya kilimo na mifugo kibiashara ndani ya nchi na nje ya nchi  pia tutaacha kuwa wazalishaji Wa malighafi kwa nchi zingine pia tutaacha kuhamasisha Elimu za viwandani kwenda nchi zingine endapo tutawekeza katika viwanda badala yake tutavuta wawekeza kutoka nchi zingine na kuja kuwekeza katika viwanda ndani ya  mikoa hii ya Kanda ya kaskazini ambapo watakuwa na uhakika Wa kupata malighafi bora za Kilimo mifugo na uvuvi

Aidha  alitoa wito kwa wakuu Wa mikoa ya Kanda ya kaskazini ,Wakuu Wa wilaya  pamoja na  wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha wanatoa huduma staiki kwa maofisa ugani  ili waweze kuwahudumia vyema wakulima na kuwajengea uwezo waweze kufikia dhamira  ya kuongeza uzalishaji ,kuongeza dhamani,pamoja na kipato katika familia  na  hatimaye kuuza kibiashara .

"Napenda kuwasisitizia wakuu Wa mikoa kuwasimamia vyema wakurugenzi Wa halmashauri  na wakurugenzi Wa halmashauri kusimamia  vyema  wakulima kulima Kilimo chenye tija pamoja na wafugaji ili kuleta chachu ya maendeleo ili wanapo uza bidhaa zao waweze kuongeza pato lao na pato la Taifa kwa ujumla "alisema Ulega

Alisema kuwa maafisa ugani  wamekuwa Wanatumika zaidi kuonyesha uwezo wao Wa nadharia zaidi katika viwanja vya maonyesho badala ya kuonyesha ujuzi wao  Wanadhari  kwa wakulima Wa vijijini . 

Kwa upande wake Mkuu  wa mikoa wa Arusha Mrisho Gambo ambaye mi mwenyeki wa maonyesho haya alisema kuwa  mwitikio kwa mwaka huu umekuwa mkubwa hususa ni kwa wafugaji tofauti na miaka ya nyuma na hata ongezeko la uongezwaji thamani mazao ya mifugo  umeongezeka .

Share To:

Post A Comment: