Monday, 21 May 2018

Serikali Yabariki Mabadiliko Kwa Vilabu,yampongeza ‘mo’ Kwa Kuwekeza Ndani Ya SimbaSerikali Yabariki Mabadiliko Kwa Vilabu,yampongeza ‘mo’ Kwa Kuwekeza Ndani Ya Simba

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe, amebariki mabadiliko ya katiba Simba ambayo yanaenda kuupokea rasmi mfumo mpya na wa kisasa wa uendeshwaji wa klabu hiyo.

Mwakyembe ameeleza hayo jana kwenye Ukumbi wa Mikutano wa JK Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam ambapo Simba walikuwa na Mkutano Mkuu wa dharura kwa ajili ya maboresho ya katiba yao.

Waziri huyo alisema ni wakati mwafaka sasa kwa klabu za Tanzania kuingia katika mfumo huu ambao umejikita kibiashara na wenye mafanikio makubwa huku akieleza kuwa haukwepeki.

Aidha Mwakyembe alimpongeza Mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo’ kwa kuamua kuwekeza ndani ya Simba akiamini ataibadilisha zaidi klabu hiyo kuweza kufika mbali kimataifa.

Baada ya kueleza hayo, Mwakyembe alisema serikali imeruhusu rasmi mabadiliko hayo kwa kuzingatia Mwekezaji lazima awekeze kwa asilimia 49 na wanachama wasalie na 51.

No comments:

Post a comment