Wednesday, 2 May 2018

Kocha Julio ashauri Tanzania iachane na Taifa Stars

Kufuatia vikosi vya timu za taifa za vijana chini ya miaka 20 na 17, Serengeti Boys na Ngrongoro Heroes, Kocha wa zamani wa Simba na Dodoma FC kwa sasa, Jamhuri Kihwelo 'Julio', ameshauri Tanzania inabidi iachane na Taifa Stars.

Akizungumza kupitia kipindi cha Spoti Leo 'Radio One', Julio ameeleza kuwa nguzu nyingi zimekuwa zikitumika kwa ajili ya Taifa stars lakini hakuna mafanikio yoyote yanayoonekana.

Julio amesema ni vema sasa nguvu hizo zilizokuwa zinapewa kwa Stars zikahamishiwa kwa timu za vijana ambazo zinaonekana kufanya vizuri kisoka.

Aidha Julio ameshauri ifikie hatua sasa Serikali iachane na Taifa Stars na badala yake zisalie timu za vijana pekee ili zipewe motisha za kuendelea kufanya vizuri kuliko Taifa Stars ambayo imekuwa haina manufaa kwa soka la Tanzania.

Usiku wa kuamkia leo kikosi cha Serengeti Boys kimewasili nchini baada ya kutwaa taji la Mashindano ya timu za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Somalia.
Mpendwa msomaji wetu, tunakukumbusha Kuidownload Application yetu ya Msumba News ili upate habari zetu kwa wepesi zaidi kama vile Magazeti kuliko ilivyo sasa.

Tumekurahisishia; 

No comments:

Post a Comment