Pep Guardiola na Liverpool kukutana na rungu la UEFA - MSUMBA NEWS BLOG

Wednesday, 11 April 2018

Pep Guardiola na Liverpool kukutana na rungu la UEFA

Shirikisho la soka Barani Ulaya, UEFA limetoa adhabu kwa meneja wa Manchester City, Pep Guardiola kufuatia kuonyesha vitendo vya utovu wa nidhamu wakati wa mchezo wao dhidi ya Liverpool uliyomalizika kwa kufungwa jumla ya mabao 2 – 1 hapo jana usiku.
Wakati huo huo UEFA imeipatia adhabu Liverpool kwa kitendo cha mashabiki wake kufanya vurugu kwa kuwasha moto na kulishambulia basi la wachezaji wa Man City wakati wa mchezo wao wa kwanza wa klabu bingwa uliyopigwa Anfield.
Guardiola ataadhibiwa kwa makosa mawili lakwanza ikiwa ni kupingana na maamuzi ya waamuzi baada ya kukataliwa bao lao la kuotea  ‘Offiside’ kitendo kilichopelekea akijikuta anavuka mstari na kuingia uwanjani na hivyo kutolewa kwenye benchi.
Kosa lapili likiwa ni kufanya mawasiliano na benchi la ufundi wakati yeye ametolewa eneo hilo hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 69 cha sheria ya UEFA.
Guardiola aliingia ndani ya uwanja wakati wa mapumziko akienda kumlalamikia mwaamuzi kwa kitendo cha kukataa bao lao ambalo lingeifanya City kuongoza kwa jumla mabao 2 – 0 kipindi cha kwanza.
Kesi hiyo itashughulikiwa na bodi inayosimamia maswala ya maadili na nidhamu ya UEFA Mei 31 mwaka 2018
Comments


EmoticonEmoticon

Notification
This is just an example, you can fill it later with your own note.
Done