Tuesday, 6 March 2018

Waziri Kigwangalla awashangaa vijana Watanzania ‘tupo bize kuangushana’


Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla amewashangaa vijana wa Tanzania kwa tabia ya kutoungana mkono kwa masuala muhimu ili kutatua changamoto zinazolikabili taifa na badala yake wanashushana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Lut. Col. Michael Mutenjele (kushoto) wakati wakivuka kivuko cha Ruvuvu wakati wa ziara yake ya kutembelea na kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo ya hifadhi katika Wilaya hiyo mkoani Kagera wiki iliyopita.
Waziri Kigwangalla amesema kuwa taifa letu linachangamoto nyingi ikiwemo ajira kwa vijana, usalama wa vyakula tunavyokula, hivyo endapo kila kijana atajitahidi kwa nafasi yake huenda changamoto hizo zikapungua na sio kazi ya kushushana.
Viongozi vijana ama wa ‘cohort’ yetu tuko bize kuangushana badala ya kuungana mkono kwenye jitihada za kutafuta suluhu za changamoto zinazoikabili nchi yetu; kuna changamoto za ajira, usalama wa chakula, mabadiliko ya tabia nchi na kadhalika. Tupambane na hizo siyo na Kigwangalla,“ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter nakuendelea kusisitiza umoja kwa vijana.
Badala ya kushambuliana na kutafuta kuangushana tushikamane kulinda maslahi ya nchi yetu, la sivyo wazee hawatokaa watuamini na kutuachia mustakabali wa nchi yetu! Hizi ni zama zetu. Tupige kazi tu!,“ameandika Waziri Kigwangalla.
Hata hivyo, Kigwangalla amewataka vijana kuachana na siasa za maji taka na kufanya siasa safi zenye maslahi mapana ya wananchi na sio maslahi binafsi.
Viongozi vijana wa zama zetu tunapaswa ku-rise above ‘politics of mediocrity’ na kufanya siasa za ‘issues’ badala ya siasa za umimi na kusaka ‘political powers’ za kibinafsi. Political powers bila kuleta tija kwenye maisha ya wananchi wenzetu ni bure!,“ameandika Kigwangalla.
Wikiendi iliyopita Waziri Kigwangalla alishambuliwa na baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii wakimtaka aombe radhi baada ya kutoa tamko la kuondolewa kwa wavamizi wa Kisiwa cha Izinga ndani ya Pori la akiba la Kimisi linalopakana na Rwanda.
Waziri Kigwangalla kwenye tamko lake alinukuliwa akisema “Kwani nyie mnashindwa kuzamisha mitumbwi yao? kitu gani kinashindikana, mtu anayevuka akija upande wetu mnamzamisha mitumbwi, manwapoteza, mkipoteza wawili watatu mnawarudisha warudi kwa kuogelea“.

No comments:

Post a Comment