Articles by "UTPC"
Showing posts with label UTPC. Show all posts

 

Chama cha Wafanyakazi katika vyombo vya habari nchini(JOWUTA) kimeitaka serikali kusimamia sheria za kazi kwa wafanyakazi katika vyombo vya habari kama zilivyo sekta nyingine ili waandishi wapate haki na stahiki zao.

Mwenyekiti wa Taifa wa JOWUTA,Mussa Juma ametoa wito huo jana wakati akizungumza katika mkutano mkuu wa Umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania(UTPC)mkoani Singida.

Juma alisema, waandishi wa habari wengi  nchini, wamekuwa wakipitia madhila makubwa ikiwepo kutoajiriwa ,kutokuwa na mikataba wala kuwa na bima za afya na Maisha.


                  MWENYEKITI JOWUTA MUSSA JUMA

"Sekta nyingine tunaona hatua zinachukuliwa kama mwajiri halipi mishahara wafanyakazi ama mwajiri anakaa na mtumishi zaidi ya mwaka bila kumpa hata mikataba"alisema

Alisema JOWUTA imejitahidi mara kadhaa kufikisha hoja za maslahi bora ya waandishi serikali lakini bado hatua hazichukuliwi za kutosha.

"Kikubwa waandishi tusiwe wanyonge,tusione taaluma hii ni watu wenye shida ,tujitokeze kutetea maslahi yetu bila hofu kwanì taaluma hii haina tofauti na taaluma nyingine katika kupata katika kazi na haki za kisheria"alisema

Juma alisema, zaidi ya asilimia 80 ya waandishi nchini hawa mikataba ya ajira wala bima jambo ambalo linapunguza ari na uhuru  wa utendaji kazi wao .

Hata hivyo, Juma aliomba wanahabari nchini kuendelea kujiunga na JOWUTA ili kuwa na sauti ya pamoja kudai haki na stahiki zao.

                                                                                                                                                                                      MKURUGENZI MTENDAJI UTPC, KENNETH SIMBAYA 

Akizungumza katika mkutano huo,Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Klabu za waandishi wa habari nchini (UTPC),Kenneth Simbaya aliomba serikali kulifanyia kazi suala la maslahi kwa waandishi wa habari.

Simbaya alimuomba aliyekuwa Mgeni rasmi katika mkutano huo,Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Adolf Mkenda kufikisha hoja za changamoto za waandishi katika baraza la mawaziri.

"Kama alivyosema awali Mwenyekiti wa JOWUTA sekta ya habari kuna changamoto nyingi tunaomba mnapokutana viongozi mlizumgumze na hili jambo la maslahi ya waandishi wetu"alisema

                 WAZIRI WA ELIMU, PROF ADOLF MKENDA

Akizungumza katika mkutano huo,Profesa Adolf Mkenda aliahidi wizara yake kushirikiana na wanahabari nchini kwani inatambua umuhimu wa vyombo vya habari.

Alisema anazijua changamoto za wanahabari ikiwepo pia suala la kitaaluma na akaahidi kushirikiana na wadau kuboresha mitaala katika vyuo vya uandishi wa habari.

Waziri Profesa Mkenda pia alizungumzia mabadiliko makubwa ya sekta ya elimu nchini ambayo yanalenga kuboresha sekta hiyo na kutoa wahitimu wenye ujuzi na uwezo kujiajiri na kuajiriwa.

                    RAIS WA UTPC, DEOGRATIUS NSOKOLO

Awali Rais wa UTPC ,Deogratius Nsokolo alitoa taarifa ya maendeleo ya utendaji ya UTPC na mikakati ijayo ya maboresho makubwa ya UTPC.

Katika mkutano huo, wanachama wa UTPC walipitisha taarifa ya mwaka,taarifa ya fedha na mikakati ijayo ya UTPC



Muungano wa klabu za waandishi wa habari Tanzania umezindua rasmi kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili ikiwa na lengo  pa kutoa elimu kwa jamii pamoja na kufikiri namna bora za kutatua changamoto mbalimbali zitokanazo na ukatili wa kijinsia hasa katika kundi la wanawake na watoto.

Akizindua kampeni hiyo mjini Morogoro mkurugenzi mtendaji wa UTPC Ndg Keneth Simbaya amesema kuwa vitendo vya ukatili wa kijisia hasa kwa wanawake na watoto ni miongoni mwa ukiukwaji mkubwa uliokithiri wa haki za binadamu na kuwataka wanahabari kushiriki vyema katika kuielimisha jamii hasa juu ya sera, sheria pamoja miongozo ambayo  itasaidia kuleta mabadiliko na kupunguza ama kuondoa kabisa ukatili.

"Waandishi wa habari kemeeni vitendo vya ukatili kwa kuandika na kuibua kila aina ya vitendo vinavyosababisha ukatili, na sii hivyo tu badala yake pia iwe sanjari na kutoa elimu kwa kuandaa vipindi pamoja na kuzipa habari zihusuzo ukatili katika vyombo vyetu vya habari". Alisema mkurugenzi.

Naye Lilian Lucas mjumbe wa bodi ya UTPC ambaye pia alimwakilisha rais wa klabu hiyo amesema kuwa baada ya kuzindua kampeni hii ni jukumu la wanahabari kutambua kuwa wanao mchango mkubwa katika kuleta mabadiliko katika jamii ikiwemo kutokomeza vitendo vya ukatili.

Kupitia kampeni hiyo, UTPC itatumia siku hizo 16 katika kutoa elimu ikiwemo kuandaa mada na mijadala mbalimbali ikiwemo ndoa na mimba za utotoni, ukeketaji na vitendo vingine kama hivyo ambavyo vimekuwa na madhara makubwa na wakati mwingine hata kugharimu maisha ya watu.

Kwa mwaka huu kauli mbiu ni Wekeza, zuia ukatili wa kijinsia.