Articles by "MWANGA"
Showing posts with label MWANGA. Show all posts

 


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Dkt Salehe Mkwizu (PhD) ametatua kero ya abiria dhidi ya wajasiriamali wachoma mahindi ambao wamekuwa na mtindo wa kutumia mabanda ya kupumzika abiria kama sehemu yao ya kuchomea mahindi. 

Mhe. Dkt Mkwizu amewaelekeza maeneo ambayo wanaweza kutumia kwa ajili ya kazi hiyo wakati mchakato wa kuandaa eneo maalum kwa ajili yao unafanyika.

Dkt. Mkwizu akiwa ameambatana na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Fedha wamewataka kuhama mara moja katika mabanda hayo kwani imekuwa kero ambapo abiria wanapata vumbi ya majivu wakati wa upepo 

Pia Mheshimiwa Mkwizu amemuelekeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kuandaa mazingira rafiki kwa kutengeneza eneo ambalo wafanyabiashara hao watakaa na kufanya biashara zao vizuri kwa kutengenezewa mabanda yenye kuwa na bati ili waweze kufanya kazi wakati wote wa mvua na jua.










Na Gift Mongi : DODOMA

Katika kuhakikisha wananchi wa jimbo la Moshi Vijijini wanapata huduma stahiki na kwa wakati mbunge wa jimbo hilo Prof Patrick Ndakidemi ameendelea kuitaka serikali kuhakikisha kunakuwepo na uhakika wa mawasiliano ya barabara.

Mbunge huyo kwa mara kadhaa amekuwa akiitaka serikali kuzijenga barabara katika jimbo hilo kwa kiwango cha lami lengo likiwa ni kurahisisha shughuli za usafirishaji na mawasiliano kwa ujumla.

Mbunge huyo amehoji Bungeni je Serikali ina mkakati gani kukamilisha barabara ya Kibosho Shine hadi kwa Rafaeli kwa kiwango cha lami.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya alisema kuwa, barabara hiyo inahudumiwa na wakala wa barabara nchini Tanroad lakini kipo kipande kinahudumiwa na wakala wa barabara vijijini Tarura.

Mhandisi Kasekenya alisema kuwa, kwa upande wa Wakala wa barabara Tanroad ni mpango wao kuhakikisha wanaijenga yote kwa kiwango cha lami na hadi sasa mkandarasi yupo eneo la mradi.

Alisema kuwa, wizara katika mwaka wa fedha 2023/2024 wametenga fedha kuendelea na ujenzi kwa awamu kwa kiwango cha lami ili kukamilisha barabara yote.

Hatua hiyo imepokelewa kwa shangwe kubwa na wananchi wa kata za Kibosho ambao wanaitegemea barabara hiyo kuwaletea maendeleo yao.

Godlisten Mallya mkazi wa Kibosho Mande alisema kupatikana kwa barabara zenye  uhakika ni kichocheo cha ukuaji wa uchumi katika eneo lao.

'Tukipata barabara ambazo zinaweza kutumika kipindi chote ni kichocheo kimojawapo katika kukuza uchumi lakini pia maendeleo yatakuja Kwa Kasi tofauti na sasa'alisema


Wananchi  wa Kijiji cha Kituri, Kata ya Kileo Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, Kilimanjaro, wameiomba serikali kuwajengea daraja la kudumu katika mto Ghona unaounganisha vijiji vya Kifaru na Kileo ili kuepukana na majanga ya vifo vinavyotokea wakati wa kuvuka.

Ombi hilo limetolewa jana na wananchi mbele ya Kamati ya Uchumi, Ujenzi na  Mazingira ambayo ilitembelea draja hilo, kujionea adha waliyonayo wananchi hao wakiwemo wanafunzi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Corman Shirima, alisema kutokana na mvua za masika kuvunja kingo za daraja na kupelekea kuharibika kwa miundombinu ya barabara na hivyo kusababisha adha kubwa kwa wananchi.

Alisema kutokana na adha hiyo ya daraja kuvunjika kingoza mto huo, wananchi wanalazimika kuzunguka hadi Kata ya Kifaru ni changamoto kwao.

Philemon Cheyo, mkazi wa kijiji cha kituri aliiomba serikali, iwasaidie kuwajengea daraja hilo kwa haraka kwa sababu ndiyo barabara kuu inayotumiwa na wanafunzi kwenda shuleni na kuwapeleka wagonjwa katika hospital ya Usangi na hospitali ya rufaa ya mkoa Mawenzi.

Diwani wa kata hiyo, Salimu Zuberi, alisema mto huo una viumbe hatari wakiwemo mamba ambao ni hatari, hivyo akaiomba serikali kupitia Wakala wa barabara TANROADS kulimimina zege daraja hilo, kwani limesababisha vifo vya watu kadhaa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Ujenzi, Mazingira, Innocent Msemo alisema wameiona adha hiyo na kwamba watakapo kwenda kwenye vikao vyao watalipa kipaumbelea daraja hilo ili kuisukuma serikali iweze kulijenga kwa haraka daraja hilo.  

Awali Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, Salehe Mkwizu alisema wanaendelea kufanya mazungumza na Wakala wa Barabara (TANROADS), ili kulipa kipaumbelea kwa kulijenga daraja hilo kwani daraja hilo ni kiungo muhimu.