Articles by "EAC"
Showing posts with label EAC. Show all posts

 • Tanzania, Rwanda na Uganda zakubaliana kusaini hati ya makubaliano ya ujenzi wa Kufua Umeme Nsongezi wa 39MW


Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati, Petroli na Madini la Jumuiya ya Afrika Mashariki umeipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kukamilisha maandalizi ya Kongamano na Maonesho ya 11 ya Petroli ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yatakayofanyika tarehe 5 hadi 7 Machi 2025 jijini Dar es Salaam.

Pongezi hizo zimetolewa kwenye mkutano wa Baraza hilo uliofanyika katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jijini Arusha.

Uenyeji wa Tanzania katika Kongamano hilo unatokana na Maamuzi ya Mkutano wa 16 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati uliofanyika Februari 14, 2024 ambao uliamua Tanzania kuwa Mwenyeji wa Kongamano na maonesho hayo.

Kongamano na Maonesho hayo ni mkakati unaolenga kutangaza fursa zilizopo katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu rasilimali za mafuta na gesi asilia na kuielezea jiolojia ya ukanda wa Afrika Mashariki ili kuvutia uwekezaji, kuendelezaji wa miundombinu, udhibiti wa uharibifu wa mazingira, usimamizi wa taarifa za mafuta na gesi asilia.

Pia linalenga kutangaza maeneo mapya ya utafutaji na kutangaza maendeleo yaliyopatikana katika sekta ya nishati katika ukanda.

Malengo mengine ni kubadilishana uzoefu kuhusu sera, sheria, kanuni na utaalamu unaotumika kwenye sekta ya nishati, kuhamasisha uwekezaji, utafutaji, uzalishaji na uendelezaji wa mafuta na gesi asilia. Vilevile Kongamano hilo linatoa fursa ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini na katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Kongamano na maonesho hayo yanatoa fursa adhimu kwa Tanzania kutangaza fursa za uwekezaji katika sekta ya Nishati hususan katika sekta ndogo ya mafuta na gesi na hivyo kuongeza wigo wa kupata wawekezaji kwenye sekta hiyo.

Mbali na hayo, Mkutano 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati, Petroli na Madini la EAC limepokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa miradi na programu mbalimbali katika sekta ya nishati, petroli na madini ikiwemo Mradi wa Kufua Umeme wa Nsongezi wenye Megawati 39 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Kagera utakaotelezwa kwa pamoja baina ya Tanzania, Rwanda na Uganda.

Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati, Petroli na Madini uliongozwa na Waziri wa Madini Mhe. Antony Mavunde (Mb.), Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga (Mb.), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi- Zanzibar Bw. Zahor Alharousy na Viongozi wengine waandamizi wa Serikali.





 


Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Bi. Veronica Nduva ameishukuru Serikali ya awamu ya sita ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kudumisha amani na utulivu nchini Tanzania, akisema suala hilo limekuwa Kivutio kikubwa cha mikutano ya Kimataifa kufanyika Mkoani Arusha na maeneo mengineyo.

Bi. Nduva ametoa kauli hiyo mapema leo Alhamisi Novemba 21, 2024 kwenye Ukumbi wa mikutano Makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakati alipokutana na wanahabari kueleza kuhusu maandalizi ya Maadhimisho ya Miaka 25 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yatakayokutanisha Wakuu wa nchi zote za Pembe hiyo ya Afrika.

Akizungumzia ratiba za Maadhimisho hayo ya Miaka 25 ya Jumuiya ya afrika Mashariki yatakayofanyika Kwenye kituo cha Kimataifa cha Mikutano AICC Jijini Arusha,  Bi Nduva ameeleza kuwa kutakuwa na Tamasha la Kitamaduni litakalojumuisha Washiriki kutoka nchi zote za EAC,huku Vikao mbalimbali vikijadili kuhusu Amani na Usalama kwa EAC pamoja na Changamoto na mafanikio ya Jumuiya hiyo.






 



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo  na Katibu  Mkuu wa Jumuiya ya Afrika  Mashariki, Bi. Veronika Mueni Nduva, alipofika Ikulu, Jijini Dar es Salaam leo tarehe 11 Novemba, 2024 ikiwa ni mara ya kwanza kukutana nae tangu Katibu Mkuu huyo aliposhika nafasi hiyo  mwezi Juni, 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema Jumuiya ya Afrika Mashariki inaweza kutumia vema idadi kubwa ya watu iliyopo hususani vijana katika kujiletea maendeleo kama itawekeza zaidi katika Elimu na Afya ya watoto.

Makamu wa Rais amesema hayo  wakati akifungua Mkutano wa Elimu wa Kikanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Sherehe za Mwaka wa Elimu wa Umoja wa Afrika 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC). Amesema ongezeko la watu katika mataifa ya Afrika Mashariki inatoa ishara ya ulazima wa kuongeza rasilimali zaidi za kifedha ili kukidhi mahitaji ya elimu bora na afya bora.

Makamu wa Rais amesema mwenendo wa idadi ya watu Afrika Mashariki inaweza kuwa baraka kubwa kwa kuendelea kuwa na vijana na watu mahiri wa kujenga uchumi ikiwa rasilimali watu hiyo itatumika kikamilifu.

Pia amesema kutokana na takwimu za Benki ya Dunia Bara la Afrika limekua likipata matokeo ya faida katika elimu ukilinganisha na mabara mengine   lakini bado ukanda wa kusini mwa jangwa la sahara, elimu imekua na ufadhili mdogo zaidi. Ametoa wito wa hatua zaidi kuchukuliwa na kutumia juhudi zote kutambua kuwa changamoto za elimu barani Afrika zinatokana kwa kiasi kikubwa na uwekezaji mdogo katika sekta hiyo, jambo ambalo linafanya kuwa vigumu kutoa elimu bora yenye ujuzi unaohitajika ili kukabiliana na maendeleo makuu matatu, ambayo ni ongezeko la idadi ya watu,utandawazi na  maendeleo ya teknolojia.

Makamu wa Rais amesema Tanzania imeendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu ambapo imelenga kufanya elimu ya lazima kutoka miaka saba iliyopo sasa hadi miaka kumi ifikapo mwaka 2027/2028. Aidha amesema mabadiliko ya mtaala wa elimu nchini yanalenga kuongeza ubora wa elimu pamoja na kuandaa rasilimali watu itakayoendana na mahitajio ya dunia ya sasa kama vile maendeleo ya dijitali, teknolojia pamoja na kutumia vema fursa mbalimbali zilizopo.

Ametaja pia hatua za uboreshaji wa miundombinu ya elimu kama vile madarasa ya kujifunzia, nyumba za walimu, kuboresha mazingira ya ufundishaji kwa kuhakikisha kuna walimu wa kutosha na nyenzo za kufundishia kama vile kompyuta na vitabu. Amesema lengo la serikali ni kuongeza ubora wa elimu, kuongeza upatikanaji wake na kuhakikisha kuwa elimu inatosheleza katika ulimwengu wa utandawazi na maendeleo ya haraka ya teknolojia.

Makamu wa Rais amewashukuru washirika wa Kimataifa wanaoiunga mkono Tanzania katika mageuzi ya sekta ya elimu na kuukaribisha mpango mpya wa ufadhili wa Umoja wa Ulaya (PEERS) ambao utasaidia uratibu wa mifumo ya elimu katika kanda. Aidha amesema Tanzania ipo tayari kufanya kazi pamoja katika mpango kazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuendeleza malengo ya kielimu.

Makamu wa Rais amesema Tanzania ina dhamira ya dhati ya kuimarisha Jumuiya ya Afrika Mashariki katika nyanja zote ikiwemo elimu.

Mkutano huo unahudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mawaziri wa Elimu na wawakilishi kutoka nchi wanachama za Afrika Mashariki, Wadau wa Maendeleo, Mashirika ya Kimataifa pamoja na Wadau wa Sekta ya Elimu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Veronica Nduva wakati alipowasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) kufungua Mkutano wa Elimu wa Kikanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Sherehe za Mwaka wa Elimu wa Umoja wa Afrika.










 


Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amewaongoza Mawaziri wa Nchi nyingine wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika uzinduzi wa Mfumo wa Kielektroniki (EAC e-Tariff Software), utakaorahisisha upatikanaji wa taarifa mbalimbali za kiforodha. 

Uzinduzi huo umefanyika wakati wa Mkutano wa 44 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Jumuiya ya Afrika uliofanyika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, Jijini Arusha.

Dkt. Nchemba alieleza kuwa kupitia Mfumo huo watumiaji watapata taarifa mbalimbali kuhusu viwango vya pamoja vya ushuru wa forodha kwa wadau wanaohusika na masuala ya kiforodha katika nchi wanachama wa jumuiya hiyo.  

Aidha, alisema kuwa Mfumo huo umelenga kurahisisha uchakataji na ufuatiliaji wa maombi ya unafuu wa ushuru wa forodha (duty remission) hivyo kupunguza urasimu pamoja na muda wa kupata huduma hizo.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, aliikumbusha Kenya, kutekeleza matakwa ya Himaya Moja ya Forodha (Single Customs Territory) ya kuweka maafisa wa forodha wa Kenya nchini Tanzania watakaofanya ukaguzi wa mizigo inayotoka ama kupitia Tanzania kwenda Kenya.

Dkt.Nchemba alieleza kuwa Tanzania imetekeleza Matakwa ya Himaya Moja ya Forodha kwa kuweka maafisa Forodha wa Tanzania upande wa Kenya takribani miaka kumi iliyopita lakini Kenya haijafanya hivyo hatua ambayo inaiathiri Tanzania katika ufanyaji wa biashara kati ya nchi hizo mbili.

Miongoni mwa athari hizo kwa upande wa Tanzania ni pamoja na kuwepo kwa kadhia ya ucheleweshaji wa mizigo inayotoka Tanzania kwenda Kenya kitendo kinachowaongezea wafanyabiashara gharama, kuwapotezea muda pamoja na msongamano katika mipaka ya Tanzania na Kenya ikiwemo Namanga, Holili, Horohoro na Sirari.

Kwa upande wake Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Kenya, Mhe. Peninah Malonza alisema kuwa Nchi yake itatekeleza Matakwa ya Himaya Moja ya Forodha na kuwaweka maafisa wake wa forodha nchini Tanzania ifikapo Julai Mosi mwaka 2024, ili kundoa vikwazo hivyo vya kibiashara.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayesimamia masuala ya Forodha, Biashara na Masuala ya Fedha, Bi. Annette Mutaawe, alisema kuwa pamoja na mambo mengine, mkutano huo umekuwa na mafanikio makubwa ambapo lengo kuu la kutano huo lilikuwa ni kujadili masuala ya kuimarisha biashara na uwekezaji katika nchi wanachama.













Serikali kupitia Wizara ya Afya imetoa mapendekezo kwa Baraza la Mawaziri wa Kisekta wa Afya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) lipitishe maombi ya Tanzania kuanzisha vituo viwili vya umahiri kwa Afrika Mashariki vitakavyotoa huduma za Afya ya Kinywa na Meno pamoja na huduma za upandikizaji Uloto. 

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema hayo leo Mei 3, 2024 kwenye Mkutano wa 24 wa Baraza la Mawaziri wa Kisekta wa Afya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika Jijini Dar Es Salaam ambapo Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wamehudhuria. 

“Chuo Kikuu cha Muhimbili kupitia idara ya kinywa na meno ina wataalamu wa kutosha pamoja na vifaa, kwa hiyo tunataka wataalamu wote wa kinywa na meno wa Afrika Mashariki waje Tanzania kujifunza katika Taasisi yetu ya MUHAS.” Amesema Waziri Ummy 

Waziri Ummy amesema Tanzania inafanya vizuri katika masuala ya upandikizaji viungo ikiwemo upandikizaji wa Uloto  hususan kwa watoto wenye changamoto za Sikoseli ambayo ni kati ya nchi Tano Duniani yenye idadi kubwa ya watoto wanaozaliwa na Sikoseli. 

Amesema, Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) tayari imeshafanya upandikizaji wa Uloto kwa watoto 10 wenye tatizo la Sikoseli na kati ya hao watoto Sita wamethibitika pasi na shaka kuwa wamepona ugonjwa wa Sikoseli. 

Aidha, Waziri Ummy amesema katika Mkutano huo wameweza kujadili kuhusu magonjwa Yakuambukiza ambapo kwa Bara la Afrika Mashariki inakabiliwa na changamoto za magonjwa ya Malaria, UKIMWI pamoja na Kifua Kikuu. 

“Sasa hivi pia tumeona ongezeko la magonjwa Yasiyoambukiza, tumeona sasa ipo haja kama  Mawaziri wa Afya wa Afrika Mashariki tuweze kuweka mikakati ya kupambana na magonjwa hayo ikiwemo kuhamasisha na kuelimisha umuhimu ww kufanya mazoezi.” Amesema Waziri Ummy 

Amesema, siri kubwa ya kuepuka magonjwa hayo ni kuzingatia ulaji wa vyakula, kupuguza unywaji wa pombe na ufanyaji wa mazoezi, kwa Tanzania kila siku ya Jumamosi kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 3:00 asubuhi imetengwa kuwa ni muda wa mazoezi ambapo Waziri Mkuu alitoa agizo la kufungwa na Daraja la Tanzanite kwa muda huo ili kuwapa uhuru watu wanaofanya mazoezi. 

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Kenya Bi. Mary Muthoni amesema Jamii inapaswa kuelimisha juu ya Afya kwakuwa Afya inaanzia nyumbani, “usipokata vichaka shida inaanzia nyumbani, usipokula vizuri shida inaanza nyumbani, usipoweka maji safi na salama shida inaanzia nyumbani”.

 


Mbunge wa Tanzania, James Millya amewataka Watanzania kuamka na kutumia fursa mbalimbali zilizopo kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Kutokana na hali hiyo amesema kupitia Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA),ambapo yeye ni Mbunge,  atahamasisha Watanzania waweze kuchangamkia fursa hizo.

Amesema yupo tayari kutembea kwenye vyuo vikuu na maeneo mengine nchini kwa ajili ya kuhamasisha mazingira mazuri ya uwekezaji, kwani ndani ya EAC kuna fursa mbalimbali haswa katika kilimo na huduma nyingine


 Na Ahmed Mahmoud


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT. Tulia Akson anatarajiwa kufungua mkutano wa kimataifa wa wabunge wa kikanda kutoka mabunge ya Afrika uliondaliwa na taasisi ya kimataifa ya Uongozi demokrasia usawa wa kijinsia IDEA LEAD AFRICA


Akizungumza na waandishi wa Habàri Mapema Leo Katibu Mkuu wa Umoja wa wabunge wanawake wa Bunge la Afrika mashariki EALA Fatuma Ndangiza amesema mkutano huo wa siku tatu utawakutanisha kujadili changamoto za kiuongozi kwa mwanamke ili kufikia malengo ya asilimia 30/30.


Amesema pamoja na changamoto pia watapeana uzoefu utakaosaidia kuongeza wigo wa viongozi wanawake ili kufikia malengo ya azimio la Beijing la kufikia walau asilimia 30 ambapo kwa Sasa imefikiwa asilimia 25 pekee.


Kwa mujibu wa Katibu huyo Fatuma Anabainisha kwamba washiriki wa Mkutano huo ni pamoja na viongozi kutoka wa mabunge ya nchi mbalimbali pamoja na kikanda ikiwemo EALA SADC ECOWAS COMESA na Afrika Magharibi Kaskazini na Kusini.


"Ni mkutano mkubwa ambao utajadili masuala ya uongozi kwa wanawake barani Afrika wanayokutana nayo ili kupata uzoefu utakaosaidia watoto wa kike kufikia malengo yao katika kuomba nafasi mbalimbali utaona hapa Afrika kwa miaka kadhaa Sasa nafasi ya Katibu Mkuu wa AU imeshikwa na wanaume pekee je hakuna Kiongozi mwanamke anayeweza kufikia huko"


Kwa Upande wake Sifisisami Dube ambaye ni Kiongozi wa IDEA LEAD Afrika amesema kwamba Taasisi hiyo ambayo inafanyakazi chini ya mwamvuli wa ubalozi wa Sweden ambapo wanalenga kazi tatu muhimu ikiwemo kusaidia masuala ya uchaguzi ushiriki wa kisiasa na kufanya masuala ya katiba katika nchi zinazohitaji kusaidiwa katika masuala hayo.


'Lakini hii wamejikita katika kitu kimoja ambacho ushiriki wa wanawake katika nyanja ya siasa pia Wana kipengele Cha vyombo vya habàri vinavyojihusisha katika ajenda mbalimbali ushikishwaji katika siasa" 

 

 

he Democratic Republic of the Congo (DRC) has today joined the East African Community (EAC) becoming its 7th Partner State.
 
The Summit of EAC Heads of State at their 19th Ordinary Summit held on Tuesday, 29th March, 2022 admitted DRC following recommendation by the Council of Ministers.

The Chairperson of the Summit, H.E Uhuru Kenyatta, who is also Kenya’s President, informed the meeting that DRC had met all the set criteria for admission as provided for in the Treaty for the establishment of the EAC.

“We have concluded the regional processes for admitting new members as provided for in our rules of procedure,” said President Kenyatta.
 
 
“Admitting DRC into EAC is historic for our Community and the African continent at large. It demonstrates the agility of the Community to expand beyond its socio-cultural boundaries to new people and trade-centered partnerships and collaboration, thus increasing trade and investment opportunities for the citizens,” added the Chair.

President Kenyatta said that he was looking forward to the DRC signing the Treaty of Accession before the stated date of 14th April, 2022.

The Summit took the decision to admit DRC into EAC after adopting the report of the Council of Ministers that had recommended the same.
 
 
Welcoming his country’s admission into the EAC, DRC President Felix Tshishekedi termed it a historical day for DRC, stating that it paves the way for the harmonization of the country’s policies with those of the EAC.

President Tshishekedi said that DRC was looking forward to increased Intra-EAC trade and reduction of tension amongst the EAC Partner States.

“It is the desire of DRC to see the creation of a new organ in the EAC that is solely focused on mining, natural resources and energy that will be based in Kinshasa, Democratic Republic of Congo,” he said.
 
 
In his remarks, Uganda’s President, Hon. Yoweri Museveni said that DRC joining the Community was an event of great significance, adding that he had personally been waiting for the last 60 years for DRC to reconnect with EAC.

“DRC has strong historical, social and cultural links with EAC Partner States. It is the onus of the EAC to now work on restoring peace and stability in Eastern DRC, a fete we can achieve by working together,” he added.
 
 
On his part, President Paul Kagame of Rwanda hailed the EAC Council of Ministers and the Summit for fast-tracking the entry of DRC into the EAC.

“I call upon EAC Organs and Institutions to accelerate the integration of DRC into the Community. Rwanda is committed to support the process,” he stated.
 
 
Speaking at the event, Tanzania’s President H.E Samia Suluhu Hassan observed that DRC has a long historical relationship with EAC.

President Samia expressed hope that DRC would ratify the Treaty of Accession to ensure full integration of her people into the bloc and reaffirmed Tanzania’s commitment to the integration process in East Africa.
 
 
On behalf of Burundi’s President H.E Evariste Ndayishimiye, Vice President Prosper Bazombanza hailed DRC President Felix Tshishekedi for the admission of his country into the Community.

“EAC projects and programmes are vital and their implementation critical for the integration process. As we move towards the Political Federation, we need to strengthen our efforts to protect our borders against terrorism, piracy and other trans-national crimes,” said the VP, as he reiterated Burundi’s commitment to constructively contribute to promoting peace and stability in the region.
 
 
Speaking on behalf of South Sudan President H.E. Salva Kiir Mayardit, Hon. Barnaba Marial Benjamin, the Minister for Presidential Affairs, hailed the entry of DRC into the EAC.

Hon. Benjamin said that his country had fallen behind in its contributions to EAC due to the prolonged armed conflict in the country and the Covid-19 pandemic.

“The President has cleared the way for all outstanding contributions to the Community,” said the Minister, even as he praised efforts to employ South Sudanese nationals into EAC Organs and Institutions.
 
 
Addressing the Summit, EAC Secretary General Hon. (Dr.) Peter Mathuki, said that the admission of DRC into the EAC comes with increased GDP and expanded market size making EAC a home to about 300 million people, which would be mutually beneficial to the people of both EAC and DRC by providing employment and investment opportunities that come along with this new development.

“The EAC now spans from the Indian Ocean to the Atlantic Ocean making the region competitive and easy to access the larger African Continental Free Trade Area (AfCFTA),” said Dr. Mathuki.

“With lower tariffs on goods and the removal of trading restrictions among Partner States, we anticipate that goods and services will move more freely. With a larger market, manufacturers in the EAC, whether large, or SMEs, will benefit from economies of scale, making them increasingly efficient and competitive,” he added.

The Secretary General invited the Private Sector to work closely with the Public Sector to tap the benefits of the entry of the central African nation into the bloc.

Further, Dr. Mathuki said that DRC’s entry also requires integrating the EAC’s trade infrastructure, intermodal connectivity, One-Stop Border Posts (OSBPs), and trade systems to reduce trade time and costs, adding that enhancing trade facilitation will enable formal and informal cross-border trade along the region’s transport corridors.

Upon ascension to The Treaty establishing the East African Community and depositing of the instrument of acceptance with the Secretary-General, DRC will join EAC’s cooperation in all the sectors, programmes and activities that promote the four pillars of EAC Integration. Collaboration in these areas will help us achieve the Community’s objectives as set out in Article 5 of the EAC Treaty