Mbunge wa Tanzania, James Millya amewataka Watanzania kuamka na kutumia fursa mbalimbali zilizopo kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Kutokana na hali hiyo amesema kupitia Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA),ambapo yeye ni Mbunge,  atahamasisha Watanzania waweze kuchangamkia fursa hizo.

Amesema yupo tayari kutembea kwenye vyuo vikuu na maeneo mengine nchini kwa ajili ya kuhamasisha mazingira mazuri ya uwekezaji, kwani ndani ya EAC kuna fursa mbalimbali haswa katika kilimo na huduma nyingine

Share To:

Post A Comment: