Na Ahmed Mahmoud


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT. Tulia Akson anatarajiwa kufungua mkutano wa kimataifa wa wabunge wa kikanda kutoka mabunge ya Afrika uliondaliwa na taasisi ya kimataifa ya Uongozi demokrasia usawa wa kijinsia IDEA LEAD AFRICA


Akizungumza na waandishi wa Habàri Mapema Leo Katibu Mkuu wa Umoja wa wabunge wanawake wa Bunge la Afrika mashariki EALA Fatuma Ndangiza amesema mkutano huo wa siku tatu utawakutanisha kujadili changamoto za kiuongozi kwa mwanamke ili kufikia malengo ya asilimia 30/30.


Amesema pamoja na changamoto pia watapeana uzoefu utakaosaidia kuongeza wigo wa viongozi wanawake ili kufikia malengo ya azimio la Beijing la kufikia walau asilimia 30 ambapo kwa Sasa imefikiwa asilimia 25 pekee.


Kwa mujibu wa Katibu huyo Fatuma Anabainisha kwamba washiriki wa Mkutano huo ni pamoja na viongozi kutoka wa mabunge ya nchi mbalimbali pamoja na kikanda ikiwemo EALA SADC ECOWAS COMESA na Afrika Magharibi Kaskazini na Kusini.


"Ni mkutano mkubwa ambao utajadili masuala ya uongozi kwa wanawake barani Afrika wanayokutana nayo ili kupata uzoefu utakaosaidia watoto wa kike kufikia malengo yao katika kuomba nafasi mbalimbali utaona hapa Afrika kwa miaka kadhaa Sasa nafasi ya Katibu Mkuu wa AU imeshikwa na wanaume pekee je hakuna Kiongozi mwanamke anayeweza kufikia huko"


Kwa Upande wake Sifisisami Dube ambaye ni Kiongozi wa IDEA LEAD Afrika amesema kwamba Taasisi hiyo ambayo inafanyakazi chini ya mwamvuli wa ubalozi wa Sweden ambapo wanalenga kazi tatu muhimu ikiwemo kusaidia masuala ya uchaguzi ushiriki wa kisiasa na kufanya masuala ya katiba katika nchi zinazohitaji kusaidiwa katika masuala hayo.


'Lakini hii wamejikita katika kitu kimoja ambacho ushiriki wa wanawake katika nyanja ya siasa pia Wana kipengele Cha vyombo vya habàri vinavyojihusisha katika ajenda mbalimbali ushikishwaji katika siasa" 

Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: