TARAFA YA IKUNGI KATA YA MKIWA


Mkuu wa wilaya ya Ikungi Ndugu Jerry C. Muro pamoja na wataalam kutoka ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri wameendelea na ziara ya utatuzi wa kero za wananchi na safari hii wamefanikiwa kutatua mgogoro wa ardhi katika kijiji cha Choda kata ya Mkiwa jimbo la singida mashariki

Dc Muro pamoja na wataalamu walilazimika kwanza kufanya mkutano wa ndani na halmashauri ya kijiji cha choda pamoja na kamati ya usimamizi wa mpango wa matumizi bora ya ardhi ya kijiji na kukubaliana kuwasilisha mpango huo kwenye mkutano wa kijiji siku hiyo hiyo hatua iliyomaliza mgogoro na mvutano wa muda mrefu

Kutatuliwa kwa mgogoro huo kumetoa nafasi kwa mwekezaji kutoka Jordan kuanza uwekezaji wa zaidi ya bilioni 12 katika wa ujenzi wa kiwanda cha kisasa kutengeneza mafuta ya alizeti, pamoja na kuanza kilimo cha alizeti ambacho kitamuwezesha pia kuzalisha mbegu za alizeti kwa ajili ya kuuza ndani na nje ya nchi katika eneo lenye hekari 1,700 katika kijiji cha choda

Dc Muro amewaomba wananchi kuufuata na kuutekeleza kwa dhati mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa kijiji cha choda mpango ambao utaondoa na kumaliza migogoro yote ya ardhi katika eneo hilo .
 


Share To:

Post A Comment: