Kamishna wa Uhifadhi - TFS Prof. Dos Santos Silayo akizungumza na wadau na wakulima wa mazao ya misiti juu ya madhara yanayotokana na moto na athari zake kwa uchumi wa jamii
Kamishna wa Uhifadhi - TFS Prof. Dos Santos Silayo akizungumza jambo na Dr Goliama wakati wa kikao cha kupambana na moto kwa wakulima wa mazao ya misitu 

 

Na Fredy mgunda,Iringa.


SERIKALI na wadau wa mazao ya misitu  wamejipanga kuhakikisha wanazuia na kuyamaliza matukio ya moto kwa kuunda mkakakati ambao utasaidia kupambana na matukio ya moto kwa wakulima wa zao hili katika wilaya ya Mufindi na wilaya nyingine zinazopakana na mkoa wa Iringa.

Kumekuwa na matukio ya moto ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara hasa katika msimu wa kiangazi ambapo mojawapo ya vyanzo vinavyotajwa na usafishaji wa mashamba kwaajili ya kuandaa mashamba.

Akizungumza wakati wa kikao hicho Kamishna wa Uhifadhi - TFS Prof. Dos Santos Silayo alisema kuwa ni wakati sasa umefika kila mmoja kutambua wajibu wake katika kuhifadhi misitu iliyopo ili ilete manufaa makubwa katika jamii yote.

"Tunashukuru nchi yetu imejaliwa kuwa na misitu yenye ikolojia mbalimbali ambayo kuna mtawanyiko kuanzia maeneo ya chini ya usawa wa bahari ambapo kuna misitu ya mikoko hadi milimani ambapo kuna misitu asili  na ile ya kupandwa inayotupa faida kiuchumi na kimazingira." Prof. Dos Santos Silayo

Hata hivyo Kamishna wa Uhifadhi ameongeza kuwa uwepo wa misitu unafaida nyingi na hivyo kila mwananchi anatakiwa kusimamia sheria zilizopo na kuona manufaa makubwa yanayopatikana kutoka katika misitu kwa kuilinda misitu iliyopo ili kuritisha vizazi vijavyo.

"Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alitoa maelekezo 15 ya kusimamia mazingira nchini na maelekezo hayo mengi yalikuwa yanahusu misitu na kwasababu hii sekta ya misitu ni sekta ambayo inasaidia sekta nyingine kukua na kuwepo kama vile upatikanaji wa maji na malighafi zitokanazo na mazao ya misitu."Prof. Dos Santos Silayo

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Saad Mtambule amewataka wananchi wa Wilaya ya Mufindi kuacha kuchoma moto hovyo katika misitu kwani kwa kufanya hivyo kunaleta madhara makubwa katika uchumi na mazingira kwa ujumla.

"Wilaya ya Mufindi tumejipanga vilivyo na hakuna mtu yoyote atakayeturudisha nyuma  katika mapambano haya ya kujikinga na matukio ya moto ili kulinda misitu yetu."Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Saad Mtambule

"Tumeona tuna adui ambaye ni mkubwa , adui moto ambaye anakatisha tamaa na kutuathiri katika jitihada zinazofanywa na wananchi kwa kupanda miti hivyo umefika mwisho wa matukio haya ya moto wilayani Mufindi na hivyo jitihada zinahitajika kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake katika kulinda misitu yetu" Mhe.Saad Mtambule

Kikao hicho kinajumuisha viongozi wote wa Wilaya, Tarafa,kata na vijiji kutoka Wilaya ya Mufindi wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Saad Mtambule.

Kikao hicho pia kinajumuisha maeneo ya yanayopakana na Shamba la Miti la Sao Hill  na wadau mbalimbali wa mazao ya misitu waliopo Wilayani Mufindi na Wilaya ya Kilombero- Morogoro na Kilolo-Iringa

Kwa upande baadhi ya Wadau walisema kongamano hilo litakuwa na manufaa makubwaa kutokana na wakulima walikuwa wanapata hasara baada ya miti yao kuungua na moto

 

Share To:

Post A Comment: