Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Mahenge akizungumza leo Juni 14, 2022 kwenye mkutano maalum wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama kwa ajili ya kupitia hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha  unaoishia Tarehe 30 Juni 2021 na Tarehe 14 Juni 2022 katika kikao kilichofanyika wilayani humo.
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mkoa wa Singida kutoka  Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Othman Jumbe akizungumza kwenye kikao hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Asia Mesos akizungumza kwenyekikao hicho.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Bosco Samwel akiongoza kikao hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo akizungumza kwenye kikao hicho.
Madiwani wakiwa kwenye kikao hicho.
Baadhi ya Wakuu wa idara wa halmashauri hiyo wakifuatilia kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Taarifa za kihasibu zikitolewa.
Madiwani wakipitia hoja za CAG.
Mkuu wa Mkoa Dk. Mahenge na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama wakipitia nyaraka zenye hoja ya CAG.
Wakaguzi kutoka ofisi ya CAG Mkoa wa Singida wakiwa kwenye kikao hicho.
Diwani wa Viti Maalum kutoka Kata ya Nduguti, Habiba Omari akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Taswira ya kikao hicho.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa wilaya hiyo, Mohamed Atiki akijibu maswali ya madiwani.
Diwani wa Kata ya Ilunda, Mohamed Imbele akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Diwani wa Viti Maalum, Zainabu Kihara kutoka Kata ya Kinyangiri  akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mkalama, Lameck Itungi akizungumza kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Diwani wa Kata ya Mwanga, Mohamed Juma akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Michango ya madiwaniikiendelea.


Na Dotto Mwaibale, Singida


MKUU wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama kwa ukusanyaji wa mapato na hiyo ni kutokana na jitihada zinazofanyika pamoja na ushirikiano wanaoufanya.

Dk. Mahenge ameyasema hayo leo Juni 14, 2022 kwenye mkutano maalum wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama kwa ajili ya kupitia hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha  unaoishia Tarehe 30 Juni 2021 na Tarehe 14 Juni 2022 ambapo alisema katika suala la ukusanyaji wa mapato hana wasiwasi wala maneno mengi kwa halmashauri hiyo kwani inafanya vizuri.

“Halmashauri ya Mkalama sina maneno mengi mnafanya kazi vizuri ya ukusanyaji mapato nina kila sababu ya kuwapongezeni “ alisema Mahenge.

Alisema moja ya kipimo cha kazi nzuri katika halmashauri mbalimbali ipo kwenye  ukusanyaji  wa mapato na kuwa mwezi wa tatu mwaka huu ilifanyika tathmini ya mapato nchi nzima na Mkoa wa Singida kwa bahati mbali ulikuwa wa mwisho ulikuwa kwenye kati ya asilimia 53 hivi au 54 lakini kati ya wilaya zaidi ya 70 zilizofanya vizuri moja wapo ilikuwa ni Mkalama na kama wilaya zingine zingejitahidi tusingekuwa wa mwisho” alisema Mahenge.

Alisema mpaka hivi sasa mavuno mengi ya mkoa wa Singida katika wilaya zote yanafanyika kuanzia mwezi wa tano na wa sita hivyo wanalazimika kubanana na kuwa anaimani watafikia asilimia 80 huku Mkalama wakiwa asilimia 95 hivyo niendelee kuwaamini leo ni tarehe 14 zimebaki wki mbili mkihimarisha ukusanyaji wa mapato katika mageti tutafikisha asilimia 100.

Katika hatua nyingine Mahenge ameendelea kupiga marufuku watu wanaojiita waganga wa kienyeji ' maarufu kama rambaramba) ambao wamekuwa wanapiga ramli chonganishi na kuchangisha fedha wakidai wanatoa uchawi na kutishia amani ndani ya wilaya hiyo kuwa waache mara moja kufanya hivyo vinginevyo watakamatwa na kufikishwa kwenye mkono wa sheria.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo alisema mpaka hivi sasa katika ukusanyaji wa mapato wamefikia asilimia 95, jumla ikiwa ni asilimia 98 na kuwa kama mvua zingekuwa zimenyesha vizuri wangekuwa wanazungumzia asilimia 120 na kueleza kuwa ukusanyaji huo umefia hatua hiyo kutokana na kazi nzuri wanayoifanya madiwani.

“Mheshimiwa mkuu wa mkoa najisikia vizuri sana kwa kazi wanayoifanya hawa madiwani kwa kweli wananiheshimisha na wanafanya kazi nzuri” alisema Kizigo.

Diwani wa Kata ya Nkindo Reuben Muhai alisema watendaji wote wanaosimamia ukusanji wa mapato wasing’ang’anie kukaa kwenye mageti badala yake waende kutafuta vyanzo vingine vya mapato vitakavyosaida kuiongezea halmashauri hiyo mapato.

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mkoa wa Singida kutoka  Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Othman Jumbe alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Asia Mesos na wenzake kwa kufanya kazi nzuri na kuwa ofisi ya CAG na wao lengo lao ni moja la kuhakikisha halmashauri hiyo inasonga mbele.

Alisema ukaguzi walioufanya mwaka juzi miradi mingi ilikuwa bado haijakamilika lakini kwa ukaguzi mwingine uliofanyika imeonesha miradi yote imekamilika hivyo anakila sababu ya kuwapongeza na kuwa viongozi wa wilaya hiyo wapo vizuri katika kufuatilia miradi na ukamilikaji wake na akatumia nafasi hiyo kuzungumzia umuhimu wa kuwa na lisiti baada ya kufanya manunuzi mbalimbali kwani lengo ni kuhakikisha kila mfanya biashara analipa kodi ya Serikali.

Katika kikao hicho hoja mbalimbali za CAG zilipitiwa na kujadiliwa na waheshimiwa madiwani ambapo Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo Bosco Samwel aliwaomba madiwani hoja zote zilizokwisha jadiliwa zisipelekwe tena kwenye kikao kijacho bali zile za sera.

 

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: