. _Amshukuru Rais Samia kwa ahadi, kutoa fedha na utekelezaji_
. _Aunga Mkono kauli ya Mhe. Rais kuwa mashindano ya AFCON ni fursa za biashara, Utalii na uwekezaji_
. _Aridhishwa na hatua za ukamilishaji wa vitu vidogo vilivyosalia_
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla, amesema ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu unaojengwa jijini Arusha kwa ajili ya mashindano ya AFCON 2027 umefikia hatua za mwisho za kukamilika, akieleza kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi pamoja na kazi za ukamilishaji wa vitu vidogo vilivyosalia.
Akizungumza leo Ijumaa, Novemba 20, 2026, wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua ujenzi wa uwanja huo, Mhe. Makalla amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutimiza ahadi, kutoa fedha na kusimamia utekelezaji wa mradi huo mkubwa ambao utaiweka Arusha katika nafasi muhimu ya kuwa mwenyeji wa mashindano ya kimataifa.
Aidha, Mhe. Makalla amesema anaunga mkono kauli ya Rais Samia kuwa mashindano ya AFCON ni fursa kubwa kwa Taifa katika kukuza biashara, utalii na uwekezaji, akieleza kuwa Arusha itanufaika kwa namna mbalimbali kutokana na wageni, mashabiki, wawekezaji na wadau wa michezo watakaofika wakati wa mashindano hayo.
Mhe. Makalla ameeleza pia kuridhishwa na hatua za ukamilishaji wa maeneo na vitu vidogo vilivyosalia katika uwanja huo, akisisitiza kuwa maendeleo yaliyofikiwa yanaonesha dhamira ya Serikali katika kuhakikisha miundombinu ya michezo inakamilika kwa wakati na kuwa tayari kwa matumizi katika mashindano ya AFCON 2027.







Post A Comment: