Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Kiuchumi Bw. Jabiri Makame amesema kuwa katika mambo ya Msingi ambayo kama Baraza tumekubaliana kuyapa kipaumbele ni pamoja na mapitio ya Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi chini ya Usimamizi wa Ofisi ya Waziri Mkuu ikiwa ni utekelezaji wa Maagizo ya Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan.

Aliongeza kuwa Sera hiyo iliandaliwa kwa kuzingatia Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025. Kwa sasa tupo katika utekelezaji wa DIRA 2050 ambayo imeweka malengo mapya na mazingira ya kiuchumi yamebadilika hivyo ni muhimu sana kuwa na Sera ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi itakayotafsiri kwa vitendo malengo ya Dira 2050.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Baraza Prof. Aurelia Kamuzora amesema kuna umuhimu wa kuanzisha Mfuko wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ili kiwe chombo cha kuwasaidia wananchi kupata mitaji, dhamana, kujengewa uwezo pamoja na kuwa kichocheo cha maendeleo ya biashara na uwekezaji
Share To:

OSCAR ASSENGA

Post A Comment: