Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Ndugu Aggrey Mwanri, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini, leo Oktoba 29, 2026, ameongoza wajumbe wa Baraza hilo kutoka vyama vya siasa vyenye usajili kamili kutembelea Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Ziara hiyo imefanyika kuelekea uzinduzi rasmi wa Mji huo unaotarajiwa kufanyika kesho, Oktoba 30, 2026, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

OSCAR ASSENGA

Post A Comment: