Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga (Mb), Agosti 24, 2026, amekutana na kufanya mazungumzo tofauti na Mabalozi wa Kenya na Afrika Kusini nchini, katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yake na Balozi wa Kenya nchini, Catherine Wahome, Waziri Kapinga amejadili namna bora ya kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya, hususan katika sekta ya biashara na viwanda.

Kapinga amesema pande hizo zimebainisha malengo ya pamoja ya kuweka mazingira wezeshi ya kibiashara yatakayochochea ukuaji wa uchumi na kuendeleza maendeleo ya mataifa hayo.

Aidha, Waziri Kapinga amekutana na Balozi wa Afrika Kusini nchini, Mhe. Noluthando Mayende-Malepe, ambapo wamejadili namna ya kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Jamhuri ya Afrika Kusini, pamoja na kuboresha mazingira ya biashara.

Mazungumzo hayo yanaonesha dhamira ya Tanzania ya kuendelea kujenga na kuimarisha mahusiano ya kiuchumi na kibiashara na nchi hizo mbili, kwa kuweka mazingira yatakayowezesha biashara, uwekezaji na maendeleo ya pamoja.
Share To:

OSCAR ASSENGA

Post A Comment: