KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo,akizungumza wakati akifungua kikao cha mwaka cha Menejimenti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo leo Julai 13,2026 jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda.

Naibu Katibu  Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Prof. Daniel Mushi,akizungumza wakati wa  kikao cha mwaka cha Menejimenti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo leo Julai 13,2026 jijini Dodoma.
  
Sehemu ya washiriki wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo,(hayupo pichani)  wakati akifungua kikao cha mwaka cha Menejimenti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo leo Julai 13,2026 jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda.

Na.Alex Sonna-DODOMA
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, ametoa maagizo matano kwa viongozi na watumishi wa sekta ya elimu nchini ili kuhakikisha sekta hiyo inaendana na mahitaji ya maendeleo ya taifa na mabadiliko ya dunia.
Prof.Nombo ametoa maagizo hayo leo Julai 13,2026 jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha mwaka cha Menejimenti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda.
Amesema mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya elimu yametokana na ushirikiano na utendaji mzuri wa viongozi na watumishi wa wizara pamoja na taasisi zake, huku akisisitiza kuwa kikao hicho ni fursa muhimu ya kutathmini mafanikio na kupanga mwelekeo wa sekta kuelekea utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
"Ndiyo maana tumeona ni muhimu kuwashirikisha wataalamu kutoka Tume ya Mipango ili kutusaidia kuona namna sekta ya elimu itakavyochangia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Tunaamini dira hiyo ndiyo itakayotuongoza katika kukidhi mahitaji ya taifa kwa miaka ijayo," amesema Prof.Nombo
Prof.Nombo ameelekeza mapitio ya mara kwa mara ya kozi na programu za elimu ili ziendane na mahitaji ya sasa ya jamii, uchumi na soko la ajira. Amesema mjadala unaoendelea katika mitandao ya kijamii kuhusu uchaguzi wa kozi kwa wahitimu wa kidato cha sita unaonesha wazi kuwa kuna mahitaji mapya ya ujuzi na taaluma yanayopaswa kuzingatiwa.
"Mrejesho tunaoupata unatufanya tujitathmini na kuangalia aina ya kozi tunazotoa ili ziendane na mahitaji ya sasa ya jamii na uchumi. Tunahitaji kuongeza ubunifu na unyumbufu katika kuwapa wanafunzi fursa ya kusoma kozi zitakazochangia maendeleo ya taifa," amesema 
Kuhusu Mfumo wa Taarifa za Usimamizi wa Elimu (ESMIS), Prof.Nombo amesisitiza umuhimu wa kuwa na takwimu sahihi kwa ajili ya kufanya maamuzi yenye tija na kuagiza taasisi zote kuhakikisha mifumo yao ya TEHAMA inaunganishwa na mfumo huo.
Amesema hatua hiyo inatekeleza maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha mifumo ya Serikali inasomana na kufanya kazi kwa pamoja, akibainisha kuwa wizara imeweka suala hilo kuwa kipaumbele.
Aidha, amehimiza kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika uwekezaji wa sekta ya elimu ili kuboresha huduma na miundombinu, pamoja na kutafuta mbinu mbadala za kugharamia sekta hiyo ili kuongeza fursa za wanafunzi wengi zaidi kuendelea na masomo.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Daniel Mushi, amewataka washiriki wa kikao kuendelea kueleza mafanikio yanayopatikana kupitia utekelezaji wa miradi na programu mbalimbali za Serikali katika sekta ya elimu.
"Hatupaswi kusita kueleza mazuri ambayo Serikali inaendelea kuyafanya kwa wananchi kwa pamoja tunaweza kuijenga sekta ya elimu yenye ushindani, ubora na tija kwa maendeleo ya taifa," amesema  Prof Mushi
Katika kikao hicho, washiriki wamepokea na kujadili mawasilisho mbalimbali ikiwemo nafasi ya elimu, sayansi na teknolojia katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, umuhimu wa mifumo ya TEHAMA katika kuongeza ufanisi wa utoaji huduma.
Vilevile,matumizi ya mfumo wa ESMIS, pamoja na Mpango Mkakati wa Wizara wa mwaka 2026/27 hadi 2030/31 na utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2026/27.
Share To:

Alex Sonna

Post A Comment: