Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Petro Magoti ameipongeza Taasisi ya Elimu Tanzania kwa namna ilivyofanya maboresho ya mitaala ya Elimu nchini yenye lengo la kumfanya muhitimu kuweza kujiajiri au kuajiriwa mara anapomaliza masomo yake.
Mhe. Magoti ameyasema hayo leo tarehe 13/7/2026 katika maonesho ya Sabasaba ambapo amesema kuwa TET inafanya kazi nzuri ya kuboresha elimu nchini.
"Kwa kweli nawapongeza kwa kazi nzuri ya kuboresha Elimu nchini hasa hivi karibuni katika maboresho ya mitaala yaliyofanyika, ni tumaini langu kwamba wanafunzi nchi nzima wataendelea kufanya vyema, "amesema mhe. Magoti.
Pia ameeleza, anafurahia namna wanafunzi wanaendelea kupatiwa vitendea kazi kama vitabu vinavyowapelekea kuendele kufanya vyema wakati wa masomo yao na kuendelea kuipongeza TET kwa uratibu mzuri na upatikanaji wa vitabu mashuleni.
TET inashiriki katika maonesho ya Kimataifa ya biashara maarufu kama Sabasaba yaliyoanza tarehe 28,Juni ambapo yanatarajiwa kufungwa hapo kesho,Julai 13.





Post A Comment: