Nilipoanzisha biashara yangu, nilikuwa na matumaini makubwa. Nilikuwa nimewekeza akiba yangu, muda wangu, na nguvu zangu zote kwenye mradi huo. Niliamini kwamba kwa kufanya kazi kwa bidii, mafanikio yangekuja haraka. Lakini mambo hayakwenda kama nilivyotarajia.

Kuanzia mwezi wa kwanza hadi wa sita, biashara yangu ilihangaika kupata faida ya kutosha. Wateja walikuwa wachache na mauzo hayakufikia kiwango nilichokuwa nimekitarajia. 

Wakati huo huo, washindani wangu walionekana kufanya vizuri zaidi kila siku. Kwa kweli nilianza kuwa na wasiwasi.

Kila mwisho wa mwezi nilipokagua hesabu zangu, niliona faida ndogo sana au wakati mwingine kutokuwepo kabisa. 

Nilijiuliza kama nilikuwa nimefanya uamuzi sahihi wa kuanzisha biashara hiyo. Kilichoniumiza zaidi ni kuona watu wakiniambia kwamba biashara yangu isingeweza kushindana na zile ambazo tayari zilikuwa zimejijengea jina sokoni.

Kadri miezi ilivyopita, shinikizo liliongezeka.

Kulikuwa na nyakati nilifikiria kufunga biashara na kutafuta jambo lingine la kufanya. Nilihisi kama juhudi zangu zote zilikuwa zinaenda bure.

Lakini sikuwa tayari kukata tamaa. Badala ya kuacha, nilianza kutafuta njia za kuboresha huduma zangu.SOMA ZAIDI.
Share To:

Post A Comment: