Katibu Mtendaji wa NACTVET Dkt.Mwajuma Lingwanda akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na kufunguliwa kwa udahili wa wanafunzi katika mwaka wa masomo 2026/2027.




Baadhi ya matukio katika picha wakati wa kutangazwa kwa dirisha la udahili mwaka wa masomo 2026/2027.

Na Mwandishi Wetu
BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) limefungua dirisha la Udahili wa wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2026/2027 kwa ngazi ya Astashahada na Stashahada katika kozi zote zinazosimamiwa na NACTVET.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma Katibu Mtendaji wa NACTVET Dkt.Mwajuma Lingwanda amesema dirisha Hilo limefunguliwa rasmi Mei 28 2026.

Amesema maombi ya udahili kwa kozi za Afya na Sayansi Shirikishi -Tanzania Bara, yatafanyika kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) unaopatikana katika tovuti ya Baraza (www.nactvet.go.tz).

Dkt.Mwajuma amesema udahili umeanza Mei 28 hadi Julai 10 2026 kwa awamu ya kwanza.

Aidha amesema maombi ya kozi zisizo za Afya na Sayansi Shirikishi, na kozi za Afya na Sayansi Shirikishi zitolewazo katika vyuo vilivyoko Zanzibar yatumwe moja kwa moja kwenye vyuo husika kuanzia Mei 28 Mei hadi Julai 10 mwaka Hui kwa awamu ya kwanza.

Hata hivyo Baraza limetoa orodha ya kozi zote na vyuo vinavyotoa kozi hizo, inapatikana katika Kitabu cha Mwongozo wa Udahili kwa Mwaka wa Masomo 2026/2027 kinachopatikana katika tovuti ya Baraza (www.nactvet.go.tz).

Baraza hilo limesema kila mwombaji kuhusika mwenyewe katika zoezi zima la kuomba kudahiliwa, kuandika taarifa zake kwa usahihi na umakini, na kutunza kumbukumbu atakazopatiwa na Baraza kupitia namba yake ya simu, bila kumpatia mtu mwingine yeyote ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza katika zoezi zima la maombi ya kujiunga na kozi katika vyuo mbalimbali.

Mambo ya Kuzingatia kwa Wanaoomba Kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System – CAS) ni Mwombaji anaweza kuomba chuo zaidi ya kimoja na Kuchaguliwa katika chuo alichoomba kutategemea ushindani utakaokuwepo katika chuo hicho.

Aidha amesema mwombaji akishachaguliwa, atapokea ujumbe kutoka NACTVET kupitia namba yake ya simu aliyoweka kwenye mfumo wakati wa kufanya maombi ujumbe utamjulisha kuwa amechaguliwa kujiunga na chuo husika na utakuwa na msimbo (code) ambao atatakiwa kuutunza na kuuwasilisha kwa chuo alichochaguliwa siku atakapowasili chuoni kwa ajili ya kuanza masomo.

Dkt. Mwajuma amesema baada ya kuwasilisha msimbo huo chuoni, atasajiliwa na chuo, kisha atapokea ujumbe kutoka NACTVET ukimweleza kuwa amesajiliwa. Baada ya kusajiliwa, mwanafunzi aingie katika tovuti ya NACTVET (www.nactvet.go.tz), kisha ajiridhishe kuwa amesajiliwa kwa kuhakiki taarifa zake kwa kubonyeza “link” inayosomeka “student’s information verification”.
Share To:

Post A Comment: