Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalum, Maryprisca Mahundi amesema maonyesho ya Mbeya City Expo yameendelea kuwa chachu ya maendeleo kwa Mkoa wa Mbeya kwa kuwakutanisha wananchi, taasisi na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Akizungumza baada ya kutembelea mabanda mbalimbali katika maonyesho hayo yanayofanyika katika viwanja vya Uhindini, Jijini Mbeya, Eng. Mahundi amesema ameridhishwa na namna shughuli za kijamii na kiuchumi zinavyooneshwa kupitia maonyesho hayo.

Amesema Mbeya City Expo imekuwa jukwaa muhimu la kutoa elimu, kutangaza huduma na bidhaa pamoja na kuhamasisha fursa za maendeleo kwa wananchi wa Mkoa wa Mbeya na maeneo ya jirani.

Aidha, amepongeza waandaaji wa maonyesho hayo kwa kutoa nafasi kwa wananchi kupata elimu na huduma mbalimbali zinazochochea maendeleo ya jamii pamoja na kukuza uchumi.

Katika hatua nyingine, Eng. Mahundi amesisitiza wananchi, hususan makundi maalum, kutumia vizuri mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na halmashauri ili kujikwamua kiuchumi na kuongeza kipato cha familia zao.

Share To:

Post A Comment: