Na Augusta Njoji

Timu ya wataalamu wa afya kutoka Hospitali ya Halmashauri ya Mji Handeni imeanza rasmi mpango wa utoaji elimu kwa jamii ili kuimarisha kinga dhidi ya magonjwa na kuboresha ustawi wa wananchi.

Utoaji wa elimu hiyo imejikita katika afua za kuzuia malaria, lishe bora, bima ya afya kwa wote pamoja na huduma za mama na mtoto, ikiwa ni sehemu ya jitihada za serikali kuhakikisha jamii inakuwa na afya bora.

Akizungumza kuhusu zoezi hilo, Ofisa Afya wa Halmashauri na Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma, Jonas Mkondya, amesema wamejipanga kutembelea kila mtaa katika kata zote 12 za Halmashauri ya Mji Handeni ili kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuwapatia elimu sahihi ya afya.

Ameeleza kuwa elimu hiyo itasaidia kuongeza uelewa kwa wananchi juu ya namna ya kujikinga na magonjwa, kuboresha lishe pamoja na umuhimu wa kujiunga na bima ya afya kwa wote ili kupata huduma kwa urahisi.

Kata zitakazofikiwa katika ziara hiyo ya wataalamu wa afya ni Konje, Mabanda, Kwenjugo, Malezi, Chanika, Mlimani, Mdoe, Vibaoni, Kwediyamba, Kideleko, Msasa na Kwamagome.

Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Alex Sonna

Post A Comment: